Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, Disemba 15, 2025 ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika Mkutano wa 18 wa Pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Usafirishaji unaofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha. Akiwa katika banda hilo, ameitaka TCAA kuendelea kuimarisha utoaji wa taarifa kwa umma pamoja na kushughulikia ipasavyo malalamiko ya wateja wa usafiri wa anga nchini.
Awali, Mhe. Kihenzile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, ambaye alimueleza kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na mamlaka hiyo, ikiwemo masuala ya udhibiti wa usafiri wa anga na utoaji wa huduma ya uongozaji ndege inayotumia mitambo ya kisasa.
Aidha, Bw. Msangi alimueleza Mhe. Kihenzile kuhusu maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), pamoja na utekelezaji wa kampeni maalum ya utoaji elimu kuhusu haki za abiria wanaotumia usafiri wa anga. Kampeni hiyo tayari imetekelezwa katika Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Julius Nyerere na Kilimanjaro, pamoja na Uwanja wa Ndege wa Arusha.
Mhe. Kihenzile alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo unaotarajiwa kumalizika Disemba 17, 2025.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Usafirishaji unaofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Banda la TCAA kwenye mkutano wa 18 wa pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Usafirishaji.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mwanamizi Elimu na Uchemuzi kutoka TCAA- CCC Debora Mligo kuhusu namna wanavyoshirikiana na TCAA katika kushughulikia malalamiko ya wateja wa utumiaji wa usafiri wa anga wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Usafirishaji
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua (kulia) mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Usafirishaji.




No comments:
Post a Comment