HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 3, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA apongeza jitihada za OCPD kujiimrisha kimifumo

 

Na: Calvin Gwabara – Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo ameipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuanzisha Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu makubwa na nyeti ya Ofisi hiyo nchini.

Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na LATRA wakifuatilia wasilisho kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA cha LATRA Mhandisi Eliud Kataraihya alieleza mtumizi ya mifumo ya kielektriniki wanayoitumia.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria walipotembelea LATRA kujifunza namna ofisi hiyo inavyotumia mifumo mbalimbali ya kielekitroniki katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku wakati wakijiandaa kuanzisha mifumo kwenye Ofisi hiyo mpya ya OCPD.

“Sisi kama LATRA tunatambua umuhimu na unyeti wa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na mmekuwa na mchango mkubwa sana katika utekelezaji wa majukumu yetu, tunawapongeza kwa kuwa Ofisi kamili na tunawahidi ushirikiano wa hali na mali ili muweze kupata kile mnachohitaji kujifunza kutoka kwetu” Alisema CPA Suluo.

Kwa upande wake Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria ambaye ameongoza menejimenti ya OCPD, Bi. Rehema Katuga ameeleza historia ya uanzishwaji wa Ofisi hiyo pamoja na majukumu yake makuu ya Uandishi wa Sheria, Urekebu pamoja na Ufasili wa sheria.

Bi. Katuga ameishukuru Serikali kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika kuimarisha Ofisi hiyo ikiwemo rasilimali watu, fedha na vitendea kazi ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa maendeleo ya taifa.

“Katika kipindi kifupi tumeweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kufanikiwa kufanya Ufasili wa sheria kuu 446 Kwa lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza ili kuwezesha watanzania wa kawaida kuweza kusoma sheria na kuzielewa vizuri lakini pia wawekezaji kuzipata kwa lugha ya kiingereza na toleo hilo litatoka hivi karibuni” alisema Bi. Katuga.

Aliongeza “Pia tulifanikiwa kutoa Toleo la Sheria zilizofanyiwa Urekebu la Mwaka 2023 na sasa tunatoa toleo la urekebu la nyongeza kila mwaka ili sheria zinapofanyiwa marekebisho zisomeke vizuri na hivyo kuwapatia watumiaji sheria zinazoenda na wakati badala ya kuwa na vipande vipande ndani ya miaka kumi ambavyo vinafanya zoezi la rejea kuwa gumu kwa watumiaji”.

Aidha amesema ziara hiyo ya mafunzo ina lengo la kuhakikisha Ofisi yao inafikia lengo la matumizi ya karatasi kuwa chini ya asilimia 10 katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiofisi na hivyo kazi zote kufanyika kupitia mifumo ya kielekitroniki na kwa haraka.

“Kutoka na uzito wa majukumu yetu mara nyingi tunakuwa tumetawanyika sana hivyo tunataka popote mtumishi atakapokuwa aweze kutekeleza majukumu ya kiofisi badala ya kulazimika kuwa Ofisini kutumia karatasi na hii itasaidia kuongeza ufanisi na tija kwa ofisi yetu na ndio maana tunataka kutumia mifumo imara na mizuri” alifafanua Bi. Katuga.

Katika ziara hii ya mafunzo, menejimenti ya OCPD pia ilitembelea Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OSG) pamoja na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na LATRA wakiwa kwenye picha ya pamoja mara bada ya kuhitimishwa kwa ziara hiyo.
MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA MAJADILIANO NA KUBADILISHANA UZOEFU













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad