HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 17, 2025

Meridianbet Yatoa Matumaini kwa Familia Zenye Uhitaji Kuelekea Krismasi

 


MERIDIANBET, kampuni kinara wa michezo ya kubashiri nchini Tanzania, imechukua hatua kubwa katika kuimarisha uhusiano wake na wateja pamoja na jamii kwa ujumla. Hatua hii inaendeleza utamaduni wake wa muda mrefu wa kurejesha fadhila kwa jamii, ambapo kampuni hiyo imetoa msaada wa vyakula na mahitaji ya msingi ya nyumbani kwa familia zenye kipato cha chini katika kata mbalimbali ndani ya Manispaa ya Kinondoni, ili kuziwezesha kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa heshima na furaha.

Mradi huu ni sehemu ya mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) wa Meridianbet, unaolenga kusaidia familia zinazokabiliwa na changamoto za maisha kwa kuwapatia mahitaji muhimu yanayoweza kuboresha ustawi wao wa kila siku. Vifurushi hivyo vimeandaliwa kwa umakini na vinajumuisha vyakula na vifaa muhimu kama mchele, mafuta ya kupikia, sukari, sabuni, vifaa vya usafi pamoja na mahitaji mengine ya msingi yanayohitajika katika maisha ya kila siku ya binadamu.

Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa msaada huo, mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisema, “Tunatambua changamoto zinazowakabili wananchi wengi katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka. Tunaamini kwamba kila familia inastahili kufurahia Sikukuu ya Krismasi kwa amani na furaha. Hii ni sehemu ya juhudi zetu za dhati kuhakikisha jamii inapata msaada wa kweli na faraja katika maisha yao ya kila siku.”

Meridianbet inaendelea kuwa kitovu cha burudani. Michezo ya kasino yenye ubora, mechi zenye odds zinazovutia, pamoja na urahisi wa kujiunga kupitia meridianbet.co.tz au *149*10# Ukiwa na Meridianbet, kila siku ni ukurasa mpya wa hadithi ya ushindi.

Wanufaika wa msaada huo kutoka Meridianbet walieleza shukrani zao za dhati, wakibainisha kuwa mgao huo umefika kwa wakati muafaka na umeleta tumaini jipya katika kipindi hiki cha sikukuu ambacho kimewakuta wengi wakiwa katika hali ngumu ya kiuchumi. Kwao, msaada huo haukuwa tu mahitaji ya msingi bali pia ishara ya kujali na mshikamano kutoka kwa kampuni inayothamini jamii inayoiunga mkono.


Mbali na zoezi hili, Meridianbet imeendelea kuonyesha dhamira yake ya muda mrefu katika kuchangia maendeleo ya jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo misaada kwa watoto yatima, maboresho ya mazingira, elimu kwa vijana, msaada kwa wagonjwa na vituo vya afya, pamoja na kampeni za michezo na burudani. Kupitia juhudi hizi endelevu, Meridianbet inaendelea kujenga misingi imara ya kusaidia jamii, ikihakikisha msaada unawafikia wale wanaouhitaji zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad