HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 8, 2025

MATUMIZI SAHIHI YA TEHEMA KUWAKOMBOA WATANZANIA KIUCHUMI

 



Na mwandishi wetu,Dar es Salaam.


WITO umetolewa kwa watanzania kufanya matumizi sahihi ya tehema katika kubuni bidhaa za kiubunifu zitakazowasaidia kuongeza kipato cha kiuchumi na kutatua changamoto mbalimbali za mazingira yanayowazunguuka.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Saaam mwishoni mwa wiki na Bw. Jason Ndanguzi akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ICT, Dkt. Nkundwe Mwasaga, katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, ikilenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na misingi ya uongozi unaoongozwa na Imani.

“Tunaposema matumizi sahihi ni kuona ni kwa namna gani tunaitumia hiyo teknolojia isiyokuwa na mipaka inayotumika duniani kote lakini katika mazingira yetu ikileta matokeo chanya kiuchumi na kijamii kitaifa, katika familia na mtu mmoja mmoja.

“Huu ni wakati unaoendana na maono makubwa ya Tanzania, kama taifa, tunaharakisha Mfumo wa Uchumi wa Kidijitali, kuimarisha Sera zetu za TEHAMA, na kuandaa watu na biashara zetu kwa mustakabali unaotegemea maarifa na teknolojia. Kwa Tume ya TEHAMA, programu hii inaonyesha kwa uwazi aina ya ujenzi wa uwezo ambao Tanzania inahitaji tunapojikita katika zama za kidijitali.

Aliongeza kuwa kwenye uchumi wa ubunifu duniani kote, muundo mmoja ni wazi, nchi zinainuka si kwa kuwa na mawazo tu, bali kwa kuwa na waanzilishi wenye uwezo, waanzilishi wenye nidhamu ya kimkakati, waanzilishi wanaoelewa teknolojia, waanzilishi wanaoongoza kwa uadilifu, waanzilishi wanaojenga biashara zinazodumu. Akasema Avoda Blue ni miongoni mwa programu chache Tanzania zinazoshughulikia hili kikamilifu.

“Kama Tume ya TEHAMA, tuko tayari kuimarisha ushirikiano na programu zinazojenga uwezo wa kidijitali, kuandaa wajasiriamali kwa ukuaji, kuunganisha teknolojia mpya, na kusaidia kuunda biashara endelevu. Ukuaji wa Tanzania unategemea wajasiriamali walio tayari kujenga kwa ujasiri, kubadilika haraka, na kuunda ubunifu usio na kikomo.

“Kwa wahitimu wetu, leo ni hatua ya mabadiliko ya utambulisho wenu. Sasa hamko tu wamiliki wa biashara, bali ni wachoraji wa mustakabali wa kidijitali na kiuchumi wa Tanzania. Katika miezi minne iliyopita, mmekuwa mkiingiliana na mifumo ya uendeshaji, nidhamu ya kifedha, zana za AI, uboreshaji wa bidhaa, kanuni za uongozi, na maandalizi kwa wawekezaji. Aina hii ya maandalizi ni nadra kwenye soko letu, na ni muhimu sana,” aliongeza Bw. Ndanguzi.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali, wakuu wa biashara, wawekezaji, na wadau wa maendeleo, Ofisa Mtendaji Mkuuu wa Unleashed Africa, Bi. Khalila Mbowe alisema programu hiyo iliyofanyika kwa ubia kati yao na Avoda Group ikianzia Uganda, imejikita zaidi katika kuwasaidia na kuwawezesha wajasiriamali wa kitanzania kutoka sekta tofauti tofauti waweze kupiga hatua kwenye biashara zao kwa uharaka zaidi.

“Kikundi cha kwanza kimewaleta pamoja waanzilishi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo teknolojia, uzalishaji wa chakula, usafirishaji, mitindo, elimu, ushauri wa mali isiyohamishika, na mashirika ya kijamii, katika miezi minne walijifunza kuhusu moduli za mtandaoni, uchambuzi wa kibinafsi, na kazi za vitendo zilizotekelezwa moja kwa moja kwenye biashara zao.

“Kwa muda mrefu, wajasiriamali wengi wa kiafrika, wakiwemo wengi wetu, tumefanya kazi kutoka pembe za nyuma za ubora wa biashara, kipindi hicho lazima kiwe historia. Katika chapa zetu zote; kutoka RiseUp, kazi ya uchumi wa ubunifu ya JUU, hadi The Space na programu yake ya kipekee ya Nipe Dili, Unleashed Africa imekuwa ikijenga mfumo kamili wa uwezeshaji ambapo vijana wanaweza kupata fursa, kukuza ujuzi wa karne ya 21, kupata msaada wa biashara, na kuimarisha uwezo wao wa uongozi ili kulipeleka mbele gurudumu la maendeleo la Taifa letu kwa kasi zaidi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050,” alisema Bi. Khalila.

Naye Mwanzilishi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu, alitoa shukrani za dhati kwa Unleashed Africa kwa kuwa shirika la kwanza Tanzania kuamini na kushirikiana na dhamira ya AVODA. Alibainisha kuwa ingawa kueneza programu hii nje ya Uganda mwanzoni ilionekana kuwa changamoto, sala za timu na mfumo imara wa ujasiriamali wa Kikristo ulisaidia kufanikisha. Aliongeza kuwa uhusiano wao na Unleashed Africa tayari unaonyesha matokeo yanayoonekana, yakithibitisha kazi yenye nguvu inayofanyika Tanzania.

“Kwa wahitimu; kwanza kabisa, mlituamini. Sasa, mnapohitimu, ni zamu yetu kuwaamini ninyi, kuhakikisha biashara zenu zinapata wateja mnaohitaji na mtaji unaohitajika. Sasa ni zamu yetu kuweka imani kwenu, nina uhakika kuwa biashara zenu zitafanikisha mambo makubwa, kweli mambo makubwa, na nasimama imara nyuma ya uhakika huo. Mahusiano ya Kikristo duniani tayari yameona na kugundua huduma zetu. Kwa kuhitimu kutoka Avoda, mmewekwa kwenye mfumo mkubwa wa kimataifa, Asia, Ulaya, na Amerika, miongoni mwa watu wanaoshiriki imani yetu na wanaotaka kuona mnafanikiwa,” alisema.

Mmoja wa wahitimu, Mhandisi Regina Fumbuka kutoka Multi Genius Africa, shirika linalolenga kufanya hesabu kuwa ya kuvutia na rahisi kufundisha, alisema kuwa programu ya Avoda imemsaidia kujifunza jinsi ya kuwa kiongozi bora, kujenga mifumo bora ya kusimamia biashara, na kuweka rekodi sahihi za kifedha. Aliongeza kuwa programu hiyo imemuwezesha kusonga kutoka kiwango kimoja hadi kingine katika safari yake ya ujasiriamali.

Ikizinduliwa mwanzoni mwa mwaka huu, AVODA Blue Tanzania ni programu ya ujasiriamali ya miezi minne yenye msisitizo kwenye utekelezaji, iliyobadilishwa kutoka Cambridge MBA na kuendana na soko la Afrika. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha dunia, ubora wa uendeshaji, na kanuni za uongozi zenye msingi wa kiimani.

Tuzo tatu zilitolewa wakati wa sherehe; Tuzo ya Utendaji Bora, Tuzo ya Ukuaji wa Biashara Bora, na Tuzo ya Uongozi wa Huduma.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Unleashed Africa, Bi. Khalila Mbowe (kulia), akiendesha mjadala katika mahafali ya programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, iliyobadilishwa kutoka Cambridge MBA na kuendana na soko la Afrika. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na kanuni za uongozi zenye msingi wa imani. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Avoda Uganda, Bw. Joshua Agonya; mmoja wa wahitimu, Bi. Esther Kolimba na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu.



Bw. Jason Ndanguzi akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ICT, Dkt. Nkundwe Mwasaga katika hafla ya mahafali ya programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, iliyobadilishwa kutoka Cambridge MBA na kuendana na soko la Afrika. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na kanuni za uongozi zenye msingi wa imani. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Unleashed Africa Social Enterprises, Bi. Ngianasia Minja (wa pili kulia), akikabidhi cheti kwa Bw. Alexander Rwiza, mhitimu wa programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na misingi ya uongozi unaoongozwa na imani. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu, na Mkurugenzi wa Avoda Uganda, Bw. Joshua Agonya.



Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Unleashed Africa Social Enterprises, Bi. Ngianasia Minja (wa pili kulia), akikabidhi cheti kwa Bi. Esther Kolimba, mhitimu wa programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na misingi ya uongozi unaoongozwa na imani. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu, na Mkurugenzi wa Avoda Uganda, Bw. Joshua Agonya.


Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu (katikati), akimvalisha ‘beji’ Bw. Elianshikira Ndossi, mhitimu wa programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na misingi ya uongozi unaoongozwa na imani. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Unleashed Africa Social Enterprises, Bi. Ngianasia Minja

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Unleashed Africa Social Enterprises, Bi. Ngianasia Minja (wa pili kulia), akikabidhi cheti kwa Bw. Charles Frank, mhitimu wa programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na misingi ya uongozi unaoongozwa na imani. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu, na Mkurugenzi wa Avoda Uganda, Bw. Joshua Agonya.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Unleashed Africa Social Enterprises, Bi. Ngianasia Minja (wa pili kulia), akikabidhi cheti kwa Bi. Ezra Makala, mhitimu wa programu ya ujasiriamali ya miezi minne ya AVODA Blue Tanzania, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Programu hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania kupitia mikakati ya kiwango cha kimataifa, ubora wa uendeshaji, na misingi ya uongozi unaoongozwa na imani. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Avoda Group, Bw. Jun Shiomitsu, na Mkurugenzi wa Avoda Uganda, Bw. Joshua Agonya.



Wahitimu wa Program ya ujasiriamali ya miezi minne ya Avoda Blue Tanzania, wakipozi kwa picha ya kumbukumbu Pamoja na wawakilishi wa waandaaji wa program hiyo, Unleashed Africa pamoja na Avoda Group, muda mfupi baada ya wahitimu hao kukabidhiwa veti vya kuhitimu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad