HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 24, 2025

HATUTAKI KUWA SOKO LA DAWA DUNI ZILIZOPITWA NA WAKATI – WAZIRI MCHENGERWA

 Na WAF – Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengrwa amesema kuwa Tanzania inajipanga kuondokana kuwa soko la dawa duni zilizopitwa na wakati na kujikita zaidi katika uboreshaji wa uzalishaji wa bidhaa za afya ndani kupitia viwanda vya ndani ya ya nchi kuvutia wawekezaji wapya wa wa Viwanda vya bidhaa za afya.

Waziri Mchengerwa amesema hayo leo Desemba 23, 2025 katika kikao cha wazalishaji wa dawa na bidhaa za afya pamoja na uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam.

”Ni lazima tuseme ukweli kwa ujasiri na kwa uwazi Bara la Afrika, na Tanzania ikiwemo, kwa muda mrefu limekuwa soko la dawa za kizazi cha zamani, dawa ambazo katika nchi zilizoendelea zimeshatumika kwa muda mrefu, baadhi yake zikibadilishwa au kuboreshwa kutokana na maendeleo ya sayansi ya tiba” amebainisha Waziri Mchengerwa.

Amesema hali hiyo imechangia Bara la Afrika kuonekana kama soko la mwisho la bidhaa za dawa, badala ya kuwa mshirika sawa katika maendeleo ya tiba ya kisasa.

”Katika mazingira haya ya utegemezi wa uagizaji, kumekuwapo pia changamoto ya dawa zisizokidhi viwango, dawa ambazo hazina kiwango sahihi cha viambato, hazijatengenezwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji, au kutokuwa na uthabiti wa ubora hadi mwisho wa matumizi” amefafanua Waziri Mchengerwa.

Amesema uwepo wa dawa duni sokoni unavuruga ushindani wa haki, wazalishaji wanaozingatia viwango, wanaowekeza kwenye ubora na teknolojia, wanajikuta wakishindanishwa na bidhaa za bei ya chini lakini zenye ubora hafifu.

”Mkakati wetu wa kukuza viwanda vya dawa vya kisasa nchini, kuhamasisha uzalishaji wa dawa za kizazi kipya, na kusisitiza viwango vya kimataifa, si ajenda ya viwanda pekee ni uamuzi wa kulinda maisha ya wananchi wetu, kuinua ubora wa huduma za afya, na kuondoa Tanzania katika mzunguko wa kuwa mpokeaji wa dawa za zamani na duni” amesema Mhe. Mchengerwa.

Amebainisha kuwa suala la kupambana na tatizo la dawa za zamani zisizoendana na mahitaji ya sasa, pamoja na dawa zisizokidhi viwango, si suala la kibiashara pekee bali ni suala la maadili, la haki ya msingi ya mwananchi kupata dawa salama na bora, na la heshima ya maisha ya kila Mtanzania.
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo Desemba 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV


Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa akizindua kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo Desemba 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV






Sehemu ya watumishi na wadau wakimsikiliza
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo Desemba 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV

















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad