Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Gerald Maganga, amesema EWURA ni mshirika mzuri katika kuisaidia TRA kutekeleza wajibu wake wa usimamizi wa kodi nchini.
“Ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, utatupeleka mbele, tuudumishe na tusimamie utekelezaji wa makubaliano yetu,” alisema.
Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma, Bwana Pendolake Elinisafi, ameishukuru EWURA kwa kuipatia TRA ushirikiano mzuri, na kuahidi kuuendeleza ili kuweka msingi imara wa mafanikio ya taasisi hizo mbili na taifa kwa ujumla.




No comments:
Post a Comment