HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 14, 2025

DC MSANDO MGUU KWA MGUU MBURAHATI UFUFUAJI VISIMA

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Mheshimiwa Abert Msando ametembelea na kukagua hali ya huduma ya upatikanaji maji kata ya Mburahati wilayani humo huku akitoa maelekezo kufufuliwa kwa visima vinne katika Kata hiyo na wananchi waanze kupata huduma ya maji.

"Leo tumeanza na kata ya Mburahati, tumepita katika visima vinne Kisiwani, Kwa Mrosso, CCM na Kwa Simba, visima hivi vina maji ambayo yanaweza kusambazwa kwa wateja na wakapata huduma, vinahitaji marekebesho madogo ambayo naelekeza DAWASA siku ya kesho Jumatatu wakamilishe maboresho hayo na visima vianze kufanya kazi," amesema DC Msando.

Msando amesema kata ya Mburahati itakua mfano wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso kukufua visima vya akiba ili kusaidia upatikanaji wa maji kwa wananchi katika kipindi hiki cha mpito wa ukame kilochopelekea kupungua kwa upatikanaji wa maji kutokana na ukame na mabadiliko ya tambia ya nchi.

"Mimi binafsi pamoja na timu ya wataalamu wa visima DAWASA tutashinda hapa Mburahati siku ya kesho kuhakikisha maagizo niliyotoa yanatekelezwa na hii itathibitisha ushirikiano mzuri kati ya serikali za mitaa, DAWASA pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kuwahudumia wananchi," amesema DC Msando.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Makama Bwire amesema maelekezo ya Mkuu wa Wilaya wameyapokea na utekelezaji wake unaanza mara moja hii leo ili ndani ya muda mfupi wananchi hawa waendelee kupata huduma ya maji.

"Lakini pia kama Mkuu wa Wilaya alivyoeleza, tukipata listi ya visima vyote katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam kutoka kwa wenyeviti na watendaji wa serikali za mitaa vilivyopo katika maeneo yao itasaidia kuvitambua kwa uharaka na kufanya maboresho ili viendelee kusaidia wananchi kuwapatia huduma ya maji," amesema Mhandisi Bwire.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad