HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 12, 2025

BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA YAZINDULIWA DODOMA

 NAIBU Waziri wa Kilimo. Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wizara ya Kilimo inaamini katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, na kuhakikisha mfumo huo unaleta manufaa zaidi kwa wakulima katika kuuza mazao yao.


Mhe. Silinde amesema hayo tarehe 12 Desemba 2025, jijini Dodoma, alivyohudhuria katika Hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala uliozinduliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb). pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, wataalam kutoa Taasisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara, wajumbe wa Bodi hiyo mpya.

Mhe. Silinde ameitaka Bodi iliyoundwa kuhakikisha inasimamia stakabadhi za ghala pamoja na kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kushiriki katika mfumo huo kwa kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na biashara.

Mhe. Silinde amesisitiza kuwa kupitia stakabadhi za ghala mazao huhifadhiwa vizuri katika viwango vinavyokidhi ubora wa masoko na hivyo kukuza kipato ca mkulima na kuongeza pato la Taifa.

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameitaka Bodi hiyo kwenda kusimamia na kuhakikisha mfumo wa stakabadhi ghalani inawanufaisha wakulima katika kuwawezesha kuhifadhi mazao yao, pamoja na kuuza katika bei nzuri kulingana na hali ya soko; pamoja na kuchagiza matumizi ya TEHAMA katika kurahisisha kazi za Bodi. Ameongeza kuwa Wizara ya viwanda na Biashara itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Kilimo kama ilivyo sasa kwa lengo la kumuinua mkulima kukuza pato lake.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad