Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Laurent Luswetila ( kulia), akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2024 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kwa Mkuu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Stivin Augustino ( wa pili kushoto) na Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa benki hiyo, Bw. Muhsin Kaye, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA. Pius Maneno.
Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Muhsin Kaye ( wa pili kushoto) akishikana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu, mara baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa pili wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2024 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Laurent Luswetila, Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno na Mkuu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Biashara wa benki hiyo, Bw. Stivin Augustino.
Mkuu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Stivin Augustino (kushoto) na Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa benki hiyo, Bw. Muhsin Kaye wakipozi mbele ya wapigapicha baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa pili wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2024, zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Stivin Augustino ( mstari wa mbele wa tatu kushoto) akipiga picha ya pamoja na washindi mbalimbali wa tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2024, zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), zilizofanyika jijini Dar es Salaam jana.

No comments:
Post a Comment