HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 18, 2025

Airtel Yazindua Teknolojia ya Airtel VoLTE Kwa Mawasiliano ya Kisasa BILA CHENGA

 




· Airtel yaja na Airtel VoLTE, wateja sasa kuperuzi na kuongea LIVE BILA CHENGA

Dar es Salaam, December 17, 2025,
KAMPUNI ya Airtel Tanzania leo imezindua rasmi teknolojia mpya ya Voice over LTE (Airtel VoLTE), hatua ambayo inaendelea kuonesha dhamira ya Airtel ya kuendelea kutoa huduma za mawasiliano ya kisesa yaani BILA CHENGA kwa wateja wake nchini kote.

Kupitia teknolojia ya Airtel VoLTE, wateja wa Airtel walio na simu janja zenye uwezo wa 4G na 5G wataweza kupiga na kupokea simu kupitia mtandao wa 4G na 5G kwa ubora wa juu na kasi zaidi, huku wakifurahia mawasiliano bora kama wako katika mazungumzo ya ana kwa ana yaani BILA CHENGA.

Tekinolojia ya Airtel VoLTE inawapa wateja uwezo wa kupiga simu huku wakiendelea kutumia intaneti bila usumbufu, jambo linaloongeza ufanisi wa huduma za kidijitali. Mbali na ubora wa sauti, teknolojia Airtel VoLTE pia inachangia kuokoa matumizi ya betri ya simu yako na kuifanya idumu zaidi na kutoisha haraka, kuongeza kasi ya kuunganisha simu na kuruhusu wateja kubadilika kutoka simu ya sauti kwa urahisi BILA CHENGA na pia bila gharama ya ziada. Mara tu huduma inapowashwa katika kifaa au simu yako yenye uwezo wa Airtel VoLTE, mteja huanza kufurahia huduma hiyo moja kwa moja bila kuhitaji usajili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, alisema kuwa kuanzishwa kwa Airtel VoLTE – BILA CHENGA ni hatua muhimu iliyopo ndani ya dhamira ya Airtel katika kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora na za kisasa. “Uzinduzi huu ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuendeleza uwekezaji mkubwa na ubunifu ili kuhakikisha mawasiliano yanapatikana kwa kasi, ubora na uhakika—kwa kifupi, mawasiliano BILA CHENGA,” alisema Kamoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhandisi wa Mtandao wa Airtel Tanzania, Prosper Mafole alisisitiza kuwa Airtel inaendeleza kuboresha na kusambaza miundombinu ya kisasa ya mawasiliano ili kuzidi kuboresha maisha ya mteja wa kawaida, wa kibiashara na wa taasisi. Alieleza kuwa Airtel VoLTE inaleta kiwango kipya cha ubora katika mawasiliano ya simu na ni sehemu ya mkakati mpana wa Airtel kuchangia kutimiza agenda ya serikali ya Tanzania ya kidijitali kutokana na kasi na ufanisi— Call- BILA CHENGA.

Uzinduzi wa teknolojia hii unaimarisha zaidi dhamira ya Airtel Tanzania ya kukuza ujumuishaji wa kidijitali, kuongeza ubora wa huduma na kuhakikisha kuwa kila mteja, awe nyumbani, kazini au kwenye shughuli za biashara, anapata uzoefu wa mawasiliano ulio imara, wa kisasa BILA CHENGA.

Vipengele Muhimu vya Airtel VoLTE:-
● Mawasiliano ya simu ya kiwango cha juu: Mazungumzo yanasikika vizuri mithili ya watu wanaozungumza ana kwa ana.

● Kuunganisha Simu kwa Haraka: Simu huunganika kwa kasi mara tatu zaidi ya mitandao ya kawaida.

● Sauti na Data kwa Pamoja: Mtumiaji anaweza kuvinjari, kutazama video au kutumia programu nyingine huku akiwa anazungumza na mtu mwingine kwa wakati mmoja.

● Matumizi Madogo ya Betri: Teknolojia hii hutumia chaji kidogo kuliko ile ya zamani.

● Video kupitia LTE: Kwa simu zinazopokea na kutumia teknolojia hii, wateja wanaweza kubadilika kwa urahisi kutoka simu ya video hadi sauti bila kutumia programu nyingine AU malipo ya ziada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad