Dar es Salaam, 19 Desemba 2025
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua rasmi kampeni ya “Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi”, kampeni ya miezi mitatu inayolenga kuhamasisha ujumuishaji wa kifedha kidijitali na kuwawezesha wateja kupitia my Airtel Money app. Kampeni hii inahakikisha kuwa kila muamala unakuwa fursa kwa wateja kwa kushinda zawadi nono pamoja na kufurahia huduma za kifedha za kidijitali zilizo salama, rahisi na za kisasa.
Kupitia kampeni ya Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi, wateja watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali. Kwa kutumia my Airtel Money app kutuma pesa, kulipa bili kupitia Lipa kwa Simu, au kununua muda wa maongezi, wateja wanajiingiza moja kwa moja kwenye droo za kushinda zawadi mbalimbali zikiwemo magari, Bajaj (magurudumu matatu), pikipiki, zawadi za fedha taslimu pamoja na kapu la zawadi za papo kwa papo kupitia activations mbalimbali.
Zawadi Kuu ni pamoja na:
● Magari 3 aina ya Mazda CX-5 – gari 1 kila mwezi kwa miezi mitatu
● Bajaj 15 (magurudumu matatu) – 5 kila mwezi
● Pikipiki 15 – 5 kila mwezi
● Zawadi za fedha taslimu – hutolewa kila wiki
● Kapu la Mizawadi la papo kwa papo – hushindaniwa moja kwa moja kwenye activations
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Airtel Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi”, Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba, alieleza lengo la kampeni hiyo akisema:
“Airtel Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi ni njia yetu ya kuwashukuru kwa dhati wateja wetu kwa kuendelea kuchagua Airtel. Zaidi ya kuthamini uaminifu wao, kampeni hii inalenga kuhamasisha matumizi ya miamala ya kidijitali iliyo salama, rahisi na yenye kuwawezesha wananchi. Kwa kutumia Airtel Money, wateja wetu wanachagua njia ya kisasa na salama ya kusimamia fedha zao huku wakipata nafasi ya kushinda zawadi kubwa. Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi inaakisi dhamira yetu ya kuwawezesha Watanzania kupitia teknolojia, kwa kurahisisha na kuongeza thamani ya miamala ya kila siku.”
Kampeni ya Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi inaonesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kuthamini uaminifu wa wateja wake, kuhamasisha miamala ya kidijitali, na kuwawezesha wateja kupitia huduma za kifedha zilizo rahisi, salama na bunifu.
Airtel inawahamasisha wateja wake pamoja na wateja wa Airtel Money kushiriki kikamilifu kwenye kampeni hii ya sikukuu kwa kupakua My Airtel Money App na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia Airtel Money ili kujipatia nafasi ya kushinda zawadi za kuvutia msimu huu wa sikukuu.


.jpeg)

.jpeg)

No comments:
Post a Comment