Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV-Bagamoyo
WAKALA wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) pamoja na Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) wameingia mkataba wa makubaliano ya kushirikiana kutoa Mafunzo ya Muda mfupi kwa Watendaji na Watumishi wa sekta ya elimu.
Waliotia saini makubaliano ya mkataba huo ni Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Maulid Maulid na Kaimu Mkuu wa Chuo SLADS Bertha Mwaihojo.Mkataba huo umesainiwa Disemba 20,2025 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba umeshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo SLADS.




No comments:
Post a Comment