HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 14, 2025

RWANDA YAIPONGEZA TANZANIA KWA USHIRIKIANO

Tanzania imepongezwa kwa kudumisha upendo na udugu miongoni mwa wananchi wa Afrika Mashariki kwa miongo mingi iliyopita.

Balozi wa Rwanda Nchini Kenya Mheshimiwa Ernest Rwamucyo ametoa pongezi hizo leo jijini Nairobi wakati alipotembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya 25 ya Wajasiriamali Wadogo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi/ Jua Kali.

Balozi Rwamucyo ambaye ni mgeni rasmi wa siku ya leo Novemba 14, 2025 maalum kwa Rwanda alisema Tanzania ni nyumbani kwa watu wengi akiwemo yeye ambayo ameishi miaka mingi na kwamba upendo na udugu toka kwa Watanzania umesaidia kuendeleza amani kwa watu wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi toka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Alana Nchimbi Pamoja na kumshukuru Balozi huyo kutembelea banda la Tanzania alikabidhi zawadi ikiwemo kitabu maalum cha historia ya Miaka 60 Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Tanzania inashiriki maonesho ya 25 ikihusisha zaidi ya Wajasiriamali 350 toka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu kupitia Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi ndio waratibu wakuu wa maonesho hayo kwa upande wa Tanzania.

Maonesho ya 25 ya Wajasiriamali Wadogo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi/ Jua Kali yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Miaka 25 ya Ujumuishaji wa Jumuiya ya Afrika MAshariki: Kuendeleza Ubunifu na Minyororo ya Thamani ya Kikanda kwa Biashara ndogo na za kati Shindani kuelekea Maendeleo Endelevu”.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad