Mgombea mteule wa udiwani kwa kata ya Butobela, Jimbo la Busanda, Wilaya ya Geita, Pascal Mapung’o, amekabidhiwa rasmi hati ya ushindi baada ya kushinda kwa asilimia 98.
Hati hiyo ya ushindi imetolewa na ,Mimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata, Hulka Saidi, katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Butobela.
Katika uchaguzi huu, jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ilikuwa 11,411, huku 11,240 wakishiriki kupiga kura. Kura zilizoharibika zilikuwa 6. Pascal Mapung’o alifanikiwa kupata kura 11,234, ambayo ni sawa na asilimia 98 ya kura zote zilizohesabiwa.
Huu ni ushindi mkubwa na wa kihistoria kwa Mapung’o na ni ishara ya kuaminiwa na wananchi wa kata hiyo.



No comments:
Post a Comment