Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Hashil Abdalah amesisitiza juu ya ukusanyaji wa taarifa sahihi ya Viwanda katika Mikoa ya Arusha na Manyara .
Dr. Harshil ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo katika Mikoa hiyo inayoanza leo tarehe 17, Novemba 2025.
Zoezi la utambuzi na ukusanyaji wa taarifa za Viwanda nchini linasimamiwa na kuratibiwa na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Katika semina hiyo ya siku Moja ,Dr.Hashil ameeleza umuhimu wa taarifa hizo Kwa Maendeleo ya Viwanda nchini kwani ndiyo dira itakayoonesha ni fursa zipi zilizopo katika Mikoa hiyo ,changamoto ,na pia kupendekesa Kwa serikali na wadau wengine wa Maendeleo nchini.
Semina hiyo imehudhuriwa pia na Viongozi wakuu wa mikoa ya Arusha na Manyara.
katibu tawala mkoa wa Manyara Bi.Mariam Muhaji amewaasa washiriki hao watakaoshiriki Moja Kwa Moja kwenye zoezi kutambua umuhimu wa zoezi hilo na kuwa wao kama mkoa wanazitegemeza sana hizo taarifa Kwa ajili ya kuweza kutambua fursa zilizopo katika mkoa wa Manyara .
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ndugu Missaile Mussa amepongeza zoezi hilo na pia kuwahakikishia ushirikiano katika kipindi chote Cha zoezi katika Wilaya na halmashauri zote za mkoa wa Arusha .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Madundo Mtambo ameeleza umuhimu wa zoezi hilo Kwa taifa Kwa ujumla.
Prof.Mtambo ameeleza kuwa zoezi la ukusanyaji wa taarifa za Viwanda lilianza katika Kanda ya Mashariki ( Dar Es Salaam , Pwani na Morogoro ) na baadaye katika Mikoa Mwanza na Shinyanga ( Kanda ya Ziwa ) na Kisha mikoa ya Tanga na Kilimanjaro ( Kanda ya Kaskazini).
Prof Mtambo ameeleza kuwa baaya kukamisha taariza za mikoa ya Arusha na Manyara watakuwa wamekamisha Kanda ya Kaskazini.
Zoezi hilo linawahusisha maafisa Biashara wa mikoa na halmashauri zote na pia maafisa Tehama Kwa ajili ya kuhakikisha uchakataji wa taarifa hizo kwenye mfumo wa taarifa unaojulikana kama NIIMS -National Industrial Information Management System ambao pia umeandaliwa na TIRDO
Monday, November 17, 2025
Home
Unlabelled
DR.HASHIL AHIMIZA UKUSANYAJI WA TAARIFA SAHIHI ZA VIWANDA KWA MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA
DR.HASHIL AHIMIZA UKUSANYAJI WA TAARIFA SAHIHI ZA VIWANDA KWA MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)











No comments:
Post a Comment