

* Yafikia mafanikio ya TZS bilioni 508 katika ufadhili wa mali
BENKI ya I&M Tanzania leo Novemba 28, 2025 imezindua rasmi huduma yake ya Asset Financing sambamba na kukabidhi magari 15 kwa mteja aliyefadhiliwa kupitia benki hiyo kwa ushirikiano na GF Automobile (Mahindra Tanzania).
Tukio hilo limeashiria hatua kubwa ya mafanikio kwa benki hiyo baada ya kufikia thamani ya TZS bilioni 508 katika mtaji wa mali ilizofadhili nchini, ikiwa ni pamoja na magari ya Mahindra na wateja wengine katika sekta mbalimbali.
Huduma ya Asset Finance ya I&M Bank Tanzania inalenga kufanya umiliki wa mali kuwa rahisi na nafuu kwa watu binafsi na biashara. Kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kupata vifaa na magari yanayozalisha kipato kwa ufadhili wa hadi 90% ya mali mpya na hadi 80% ya mali iliyotumika, huku wakiwezeshwa kulipa kwa kipindi kinachofikia hadi miezi 60.
Akizungumza katika hafla hiyo, Simon Gachahi, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi wa I&M Bank Tanzania, amesema: “Leo tunajivunia kukabidhi magari ya Mahindra ambayo yataanza kazi mara mojakusafirisha bidhaa, kusaidia miradi ya ujenzi na kuchochea shughuli za kiuchumi nchini. Kufikia TZS bilioni 508 katika mali tulizofadhili, na Mahindra Tanzania tukiwa mmoja wa washirika wetu wa kuaminika, ni ushahidi kuwa huduma yetu ya Asset Finance inaleta maendeleo halisi.”
“Ushirikiano wetu wa kimkakati na Mahindra Tanzania unaleta pamoja magari bora na ufadhili rahisi, wa haraka na wa kiwango cha juu kutoka I&M Bank. Ushirikiano huu unaondoa vikwazo kwa biashara kupanua mabehewa yao na kuwafanya wateja wetu wakue kwa ujasiri na kasi. Matukio kama la leo ni uthibitisho wa mafanikio yanayopatikana pale mali bora zinapokutana na ufadhili unaomzingatia mteja.” Amesema Gachahi
Akizungumzia kuhusiana na huduma hiyo amesema imeundwa mahsusi kusaidia wateja na washirika kama Mahindra Tanzania kupata mali zinazozalisha kipato kama vile magari ya biashara, mitambo na vifaa mbalimbali katika sekta za usafirishaji, ujenzi, uzalishaji, kilimo, madini, usafirishaji na utalii.
Mpaka sasa, benki imefadhili mali kufikia jumla ya TZS bilioni 508, ikiwa na manufaa kama, Ufadhili wa hadi 90% kwa mali mpya na 80% kwa mali iliyotumika, kipindi cha marejesho hadi miezi 60 kwa wateja binafsi na miezi 48 kwa biashara, riba shindani na mchakato wa uidhinishaji wa haraka, bima kamili na mfumo wa ufuatiliaji kwa usalama na huduma makini kutoka kwa maafisa mahusiano na timu za matawi.
Amesisitiza kuwa benki I&M Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kupanua mtandao wa wauzaji, kuanzisha huduma bunifu kama mikopo ya mzunguko (revolving credit), na kuendelea kuwa mshirika wa kuaminika kwa Watanzania wanaotaka kumiliki mali kwa ajili ya kukuza kipato na biashara.
Naye Mkurugenzi wa mauzo kutoka kapuni ya GF Automobile Mujtaba Karmali ameishukuru serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini ambapo wanatarajia kuanzisha kuwanda cha kuunganisha magari na hivyo kuiomba serikali kutoa kipaumbele kwa makuampuni ya ndani ili kuongeza wigo wa ajira na kukuza mapato ya serikali.
Tumefurahi sana kushirikiana na Benki ya I&M pamoja na Synarete katika kufadhili mteja wetu mkubwa, ambaye amenunua magari 26 yanayoweza kufanya kazi katika mazingira yoyote.
Tunatarajia kuendeleza ushirikiano huu kwa manufaa ya wateja wetu na maendeleo ya sekta ya usafirishaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Synarete, Deep Joshi ameishukuru GF Automobile pamoja na Benki ya I&M kwa ushirikiano mzuri uliowezesha wadau wote kuweka malengo sawa katika kufanikisha upatikanaji wa magari maalum kwa ajili ya kuwawezesha mainjinia wa minara jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa magari hayo mapya yatawawezesha mainjinia kutoa huduma bora, za haraka na za uhakika kwa wakazi wa Dar es Salaam, hivyo kuunga mkono jitihada za kuboresha miundombinu ya mawasiliano na huduma muhimu kwa jamii.
Ametamatisha kwa kusisitiza kuwa Synarete itaendelea kushirikiana na wadau wake ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa za kiwango cha juu na zenye tija kwa wananchi.



No comments:
Post a Comment