Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA mkoa wa Geita ametia saini ujenzi wa miradi minne ya maji katika wilaya za Geita, Chato na Mbogwe yenye thamani ya jumla sh. bilioni 3.6.
Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita Jabir Kayila amese makuwa takribani wananchi 27000 kutoka katika vijiji 12 katika wilaya tatu za mkoa wa geita wanatarajiwa kunufanika na miradi pale itakapo kamilika.
Vijiji vinavyoenda kufikiwa na miradi hii ni pamoja na Lwezera, Ikina, Bugogo, Ihega, Nyarugusu, Rumasa, Manila,Ngemo,Bwendamwizo, Ilolangulu, Bunigonzi na Mpakali.
Miradi hii inatarajiwa kwenda kuongeza hali ya upatikanaji wa maji vijijini kwa asilimia 4 ambapo hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijijini kwasasa ni zaidi ya asilimia 70 hivyo kupitia miradi hii hali ya upatikanaji wa maji inatarajiwa kufikia asilimia 86 na kuvuka lengo.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela ametoa rai kwa wakandarasi waliosaini mikataba hiyo kwenda na wakati ili waweze kumaliza miradi hiyo na wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo.
No comments:
Post a Comment