HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 17, 2025

TANROADS INAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BILIONI 383 MKOANI MBEYA

Serikali inaendelea na Ujenzi wa Barabara ya Njia Nne (Dual Carriageway) 29km Kuanzia Uyole (Nsalaga) hadi Ifisi yenye urefu wa kilomita 29, mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi M/s China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) huku Mhandisi Mshauri akiwa ni TECU kwa gharama ya shilingi Bilioni 138.727 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT) yenye thamani ya Bilioni 24.970.

Serikali inaendelea na mradi wa Ukarabati kwa Kiwango cha lami Barabara ya Ibanda – Kiwira Port (Km28.0) na Kajunjumele – Itungi Port (Km 4.0) unaojengwa kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 38.359 bila nyongeza za thamani (VAT) na ulikua unatekelezwa na Kampuni ya AVM-Diligham ya Uturuki ambaye kutokana na kuchelewesha kazi mkataba wake ulivunjwa mnamo tarehe 9 Mei 2024 na sasa taratibu za kumpata mkandarasi mwingine zinaendelea.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 17 Octoba 2025 na Meneja TANROADS Mkoa wa Mbeya Mhandisi Matari Masige ofisini kwake Jijini Mbeya wakati akieleza taarifa ya Utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maendeleo inayotekelezwa na TANROADS mkoani hapo.

Pia serikali inaendelea na mradi wa Ujenzi wa jengo jipya la abiria (terminal building) katika uwanja wa ndege wa Songwe ambapo Ujenzi wa jengo la abiria (Terminal Building) umekamilika ukiwa umetekelezwa na Mkandarasi M/s China Geo- Engineering Corporation kwa gharama ya bilioni 14.118 bila kodi na unasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/s UNETEC kutoka Dubai na kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA)

Mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma ya Pamoja mpakani (OSBP) katika eneo la kasumulu/Songwe katika mpaka wa Tanzania na Malawi unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo awali Serikali ilipata mkopo kutoka Benki ya Dunia, Mradi unatekelezwa na mkandarasi M/s China Geo Engineering Corporation (CGC), Mradi huu wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania bilioni 26.426 unajengwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ambaye ndiye mwajiri na ulisimamiwa na kampuni ya kihandisi ya ECG Engineering Consultant Group S.A ya Misri ikishirikiana na Wakala wa Majengo (TBA).

Mradi mwingine ni wa Ujenzi wa barabara ya Katumba – Mbambo – Tukuyu (km 83) kwa kiwango cha lami, sehemu ya Bujesi - Mbambo (km10) na Tukuyu – Mbambo (km 7) hata hivyo Barabara hiyo imegawanywa katika sehemu kuu tano ambazo ni Sehemu ya Katumba – Lupaso, km 35.3, Sehemu ya Lupaso – Bujesi, km 10.0, Sehemu ya Bujesi - Mbambo, km10.0, Mbaka – Kibanja, km 20.7 na Kibanja – Tukuyu, km 7.0 “Sehemu ya (ii), (iii) na (V) zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Sehemu iliyobakia ya Katumba – Lupaso (km 35.3) na Mbaka – Kibanja (km 20.7). Serikali tayari imesaini mkataba na mkandarasi M/s China Road Construction and Bridge Corporation ya China kwa gharama ya shilingi Bilioni 86” Amesisitiza

Pia Ujenzi wa barabara ya Katumba – Mbambo – Tukuyu (km 79.4) kwa kiwango cha lami, sehemu ya tatu; Katumba - Lupaso (km 35.3) Lot 3 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 54.085 bila nyongeza za thamani (VAT) na utatekelezwa na Kampuni ya M/s China Road Construction and Bridge Corporation ya China na sehemu ya nne; Mbaka – Kibanja (km 20.7) Lot 4 kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 32.041 bila nyongeza za thamani (VAT) na utatekelezwa na Kampuni ya M/s China Road Construction and Bridge Corporation ya China.

Mhandisi Masige amesema kuwa mradi mwingine ni wa barabara ya Igawa – Tunduma (km 218) na Uyole – Songwe (Bypass) km 48.9 (PPP) Contract ambao ni moja ya mikakati endelevu ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nyanda za juu kusini na Nchi za kusini mwa Afrika, Mfano. Zambia, DRC n.k kwa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji. Mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa ubia wa Serikali na Sekta binafsi yaani PPP (Public, Private, Partership).

Mhandisi Masige amesema kuwa serikali inaendelea na utekelezaji wa kazi za ujenzi wa madaraja ya dharula CERC PROJECT) ikiwa ni ni moja ya mikakati ya serikali kuzuia kujirudia kwa maafa ya mafuriko yaliyojitokeza kipindi cha mvua kubwa za El-Nino (2023/24) zilizosababisha uharibifu mkubwa kwenye miundombinu ya Barabara nchi nzima na kuathiri uchumi unaozalishwa kupitia sekta ya usafiri na usafirishaji na kwa Mkoa wa Mbeya inatekeleza miradi mitatu yenye jumla ya Shilingi Bilioni 19.5

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni Pamoja na ujenzi wa Daraja la Songwe katika Barabara kuu ya TANZAM linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 9,532, Ujenzi wa Daraja la Lupatingatinga katika Barabara kuu ya Mbeya – Rungwa (Mbeya/Singida brd) linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 5,671 na Ujenzi wa Daraja la Bitimanyanga katika Barabara kuu ya Mbeya – Rungwa (Mbeya/Singida Brd) linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 4,369






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad