HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 12, 2025

TADB YASHIRIKI UZINDUZI WA WIKI YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA MKOANI TANGA

Wiki ya Maadhimisho ya Chakula Duniani Kitaifa imefunguliwa rasmi leo tarehe 11 Oktoba 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Batilda Buriani, katika viwanja vya Usagara jijini Tanga.

 Maadhimisho haya yataendelea hadi tarehe 16 Oktoba 2025, yakihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya chakula kutoka ndani na nje ya nchi.

Kauli mbiu ya mwaka huu “Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora kwa Maisha ya Baadaye” inaweka msisitizo wa kitaifa juu ya mshikamano, ubunifu, na uwajibikaji wa pamoja katika kujenga mifumo endelevu ya usalama wa chakula kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kama mdau muhimu wa sekta ya chakula, inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa chakula. 

Kupitia mikopo nafuu kwa wakulima, waongezaji thamani, na watoa huduma katika mnyororo wa thamani ya kilimo, TADB inachochea mapinduzi ya kilimo cha kisasa kilimo chenye tija, chenye thamani ya kibiashara, na chenye kuleta ustawi wa jamii.

Katika maadhimisho haya, TADB imesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo kinachojenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. 

Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, benki inaendelea kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa chakula bora, salama, na chenye lishe kwa Watanzania wote—kwa sasa na kwa baadaye.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad