HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 3, 2025

Mwenyekiti Baraza la Uongozi NACTVET ashuhudia utoaji mafunzo ya amali shule za Sekondari

 

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTVET, Bi. Bernadetta Ndunguru akipata maelelezo kutoka kwa Mwalimu na Mratibu wa Mafunzo ya Amali katika Shule ya Sekondari Dar es Salaam wakati alipotembelea Shule hiyo kuangalia ubora wa Mafunzo yanayotolewa.
Wanafunzi wa Kidato cha Pili Shule ya Sekondari Dar es Salaam wakionesha ujuzi wa ushonaji katika mkondo wa mafunzo ya Amali.

Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Baraza la Uongozi NACTVET, Bi. Bernadetta Ndunguru, ametembelea shule za sekondari zinazotoa mafunzo ya amali kujionea maendeleo ya utoaji mafunzo hayo katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Ndunguru, amesema kuwa NACTVET imeendelea kutekeleza jukumu la kusimamia ubora wa mafunzo katika shule hizo kwa lengo la kuzalisha wahitimu wenye ujuzi stahiki.

Amesema kuwa utekelezaji wa mafunzo ya Amali kwa shule za Sekondari umekuwa na mwitikio chanya kwa wanafunzi katika kujipatia ujuzi na maarifa fursa za ajira mara baada ya kuhitimu
Amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, imewekeza kikamilifu katika mafunzo ya Amali na matunda yake yameanza kuonekana kupitia kazi mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi wanaonufaika na mafunzo hayo katika shule mbalimbali nchini.

“Dhamira ya Serikali ya kuanzisha Mkondo wa Amali katika shule za Sekondari  ni kuwandaa vijana kuwa na ujuzi katika fani mbalimbal,utakaowajengea msingi wa kujipatia ajira mara baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari ,” amesema

Kwa upande wake, Meneja wa NACTVET Kanda ya Mashariki, Dkt.Hirst Ndisa, amesema kuwa NACTVET inaendelea kushirikiana kwa karibu na shule hizo ili kuimarisha ubora na ufanisi wa utoaji mafunzo.  

Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari Dar es Salaam, Bw. Hussein Njau, ameishukuru Serikali kwa kuwezesha utoaji wa mafunzo ya amali ambayo yamekuwa chachu kwa wanafunzi kujipatia ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiriwa.

Mwanafunzi wa fani ya Ufundi Umeme katika shule ya Sekondari Baobab, Careen Jonathan, amesema kuwa kupitia mafunzo ya amali anaamini kuwa atakuwa na uwezo wa kufanya kazi mbalimbali za kitaalamu katika fani hiyo mara baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne.

Ameongeza kuwa kadri wanavyoendelea na mafunzo hayo, wanazidi kupata umahiri na ujuzi katika fani zao, jambo linalowasaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii na hivyo kujipatia fursa za ajira.


Wanafunzi wa Kidato cha Pili Shule ya Sekondari Dar es Salaam wakionesha ujuzi wa ushonaji katika mkondo wa mafunzo ya Amali.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTVET, Bi. Bernadetta Ndunguru akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa  Shule ya Sekondari  Baobab Mwalimu na Mratibu wa wakati alipotembelea Shule hiyo kuangalia ubora wa Mafunzo yanayotolewa shule hiyo .
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi NACTVET, Bi. Bernadetta Ndunguru akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa  Shule ya Sekondari  Baobab Mwalimu na Mratibu wa wakati alipotembelea Shule hiyo kuangalia ubora wa Mafunzo yanayotolewa shule hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab  wakiwa mafunzo ya Amali katika Shule hiyo.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad