Mgombea udiwani wa Kata ya Nyanguku Elias Ngole kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo wamembatiza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini,Mhandisi Chacha Wambura jina la ‘NZAGAMBA’ jina la kisukuma ikimaanisha Ng’ombe mwenye mabavu au shujaa ambae watarajie Mgombea huyo Mhandisi Wambura atawasimamia kikamilifu na kuwa msemaji wa wananchi wa jimbo hilo.
Ngole amesema hayo wakati wa kampeni ya Udiwani katika eneo la Kijiji cha Nyanguku iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Geita ambapo amemuomba kuwatatulia kilio cha ujenzi wa barabara kutoka Buhalahala kuelekea Nyakato yenye urefu wa Kilomita NANE na amesema uboreshaji wa barabara hiyo utasaidia kuboresha huduma na shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa maeneo hayo.
Ngole ameomba pia suala ya ujenzi wa Chuo Kikuu kata hiyo ina eneo kubwa la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini,Mhandisi Chacha Wambura amesema amelipokea jina hilo na atasimamia kutokana na sifa ya jina la ‘NZAGAMBA’ aendane na matakwa ya sifa zilizoainishwa kwa jina hilo hasa kuhusu Ushujaa na Mabavu ili kuwa msemaji wa wananchi pindi atakapochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,Tarehe 29 Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo Mgombe Ubunge huyo kupitia Chama cha Mapinduzi,Mhandisi Wambura amewahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura siku hiyo na kuchagua mafiga matatu akimaanisha kuanzia nafasi ya Urais wamchague Mgombea wa kiti hicho,Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN,Ubunge yeye mwenyewe Mhandisi Chacha Wambura na nafasi ya Udiwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole.
No comments:
Post a Comment