HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 14, 2025

Meridianbet Yadhamini “Chanika Veteran Bonanza 2025” Kuunga Mkono Michezo



KWA mara nyingine tena, Meridianbet imeonyesha dhamira yake ya dhati katika kusaidia jamii kupitia michezo, kwa kudhamini mashindano ya “Chanika Veteran Bonanza 2025”, tukio kubwa linalowakutanisha wapenzi wa soka na wachezaji wastaafu kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Kupitia udhamini huu, Meridianbet imechangia jezi kamili kwa timu shiriki, mipira ya michezo, pamoja na zawadi maalum kwa mshindi wa bonanza hili, kama sehemu ya mpango wake endelevu wa kurudisha kwa jamii (CSR). Hatua hii inalenga kuunga mkono juhudi za kukuza michezo ya jamii, kukuza vipaji, na kuimarisha umoja kupitia burudani ya soka.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, mwakilishi wa Meridianbet alisema:

“Sisi kama Meridianbet tunaamini kuwa michezo ni zaidi ya burudani. Ni jukwaa la kuunganisha jamii, kuibua vipaji na kuhamasisha afya bora. Ndio maana tumeamua kushirikiana na kamati ya Chanika Veteran Bonanza kuhakikisha tukio hili linafanyika kwa kiwango cha juu.”

Meridianbet pia inakuletea michezo ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Bonanza hilo linatarajiwa kushirikisha timu mbalimbali za wachezaji wastaafu na vijana, likiwa na lengo la kuimarisha mahusiano kati ya vizazi tofauti kupitia mchezo wa soka. Zaidi ya kuwa na ushindani wa kiurafiki, tukio hili limekuwa sehemu ya ratiba ya michezo inayosubiriwa kwa hamu kila mwaka na wakazi wa Chanika na maeneo jirani.

Kamati ya maandalizi ya Chanika Veteran Bonanza imeishukuru Meridianbet kwa udhamini huu muhimu, hususan katika kipindi ambacho wadau wa michezo wa ndani wanahamasishwa kushiriki kikamilifu kuinua michezo ya jamii.

“Udhamini huu umetupa nguvu kubwa. Tunashukuru sana Meridianbet kwa kuona thamani ya bonanza letu na kuamua kuwa sehemu ya mafanikio haya. Vifaa hivi vitachangia kuboresha ushindani na kuleta hamasa zaidi kwa washiriki,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza.
Meridianbet itaendelea kushirikiana na jamii katika maeneo mbalimbali nchini kwa miradi ya kijamii yenye kugusa maisha ya watu moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, michezo na mazingira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad