Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Familia moja mjini Bukoba ipo katika huzuni kubwa baada ya kijana wao, Anordius Angelius Rweikiza (16), mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Bukoba Lutheran Secondary School (BLSS), kuripotiwa kupotea tangu Jumatano, Oktoba 7, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Katibu wa Bikorwa Engonzi, Anordius alionekana mara ya mwisho akiwa shuleni huku akiwa amevaa sare za shule na hadi sasa hajulikani alipo.
Baba mzazi wa kijana huyo, Angelius Rweikiza, amesema familia kwa kushirikiana na ndugu na marafiki imeanza jitihada za kumtafuta, huku yeye akielekea Bukoba kuungana na mamlaka husika katika msako.
“Tuna hofu kubwa kwa kuwa ni kijana mdogo bado yupo shuleni. Tunaomba yeyote mwenye taarifa zozote zitakazosaidia apige simu mara moja ili tumpate salama,” alisema Rweikiza.
Aidha, familia imetoa namba za mawasiliano kwa yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kufanikisha upatikanaji wake: 0782 048 123 au 0741 114 398.
Hadi sasa mamlaka za usalama bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu kupotea kwa kijana huyo.
No comments:
Post a Comment