HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 19, 2025

KAIRUKI AAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU, AFYA NA URASIMISHAJI MSIGANI

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angellah Kairuki, ameendelea na kampeni zake kwa kishindo katika Kata ya Msigani ambapo amewaahidi wananchi kushughulikia changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili kata hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Zone, Kairuki alisema kipaumbele chake ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu karibu na makazi yao, ikiwemo ujenzi wa zahanati na shule ya sekondari katika maeneo yanayokosa huduma hizo.

Aidha, ameahidi kufuatilia kwa karibu mchakato wa urasimishaji wa ardhi ili kuhakikisha wananchi wanamilikishwa ardhi kwa haki, uwazi na utaratibu unaoeleweka.
Katika sekta ya miundombinu, Kairuki aliahidi kutatua changamoto ya vivuko katika maeneo ya Kwa Mkama, Kwa Daba, Kwa Mariam, Ukombozi Tanesco, Zone na maeneo mengine, kwa kuweka vivuko bora vitakavyokidhi mahitaji ya wakazi.

Kuhusu usalama wa wananchi, mgombea huyo alisema atasimamia uanzishwaji wa kituo cha polisi katika mitaa ya Msingwa na Malamba Mawili ili kuimarisha hali ya ulinzi na kupunguza matukio ya uhalifu.

Amewaomba wananchi wa Msigani na jimbo lote la Kibamba kumpa kura katika uchaguzi ujao ili aweze kulivalia njuga bungeni tatizo la huduma za kijamii na miundombinu, na kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad