HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 15, 2025

EZEKIA WENJE AZIDI KUIMBUA CHADEMA MBELE YA DK.SAMIA

*Asema mapendekezo yote waliyoyatoka yamefanyiwa kazi lakini wamekimbia uchaguzi

*Asema ni hatari kuwa na kiongozi anayesema yuko tayari kufa,Asisitiza Oktoba ni kutiki 


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kagera.

ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kwa miaka 15 ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kanda ya Ziwa Ezekia Wenje amekiumba Chama chake cha zamani.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan,Wenje ambaye kwa sasa amejiunga CCM amesema CHADEMA wamekimbia Uchaguzi mkuu kwa kuweka mpira kwapani.

Wenje amesema baada ya Dk.Samia kuingia madarakani aliwaita wadau wa siasa wakiwemo CHADEMA kujadiliana namna bora ya kuimarisha demokrasia nchini.

“Tunakumbuka Dk.Samia baada ya kuingia madarakani, ulituita mezani kuja kuzungumza. Katika kikao kile ambacho kulikuwa na viongozi kutoka vyama vya siasa na wadau wa siasa lakini CHADEMA tulikataa.

Pamoja na CHADEMA kutoshiriki katika mikutano ya kushughulikiq changamoto za kisasa kupitia Kikosi kazi kilichoundwa na Rais Dk.Samia bado mapendekezo yao yalifanyiwa kazi

“CHADEMA tulikuja na mahitaji yetu ambapo kwanza tukaomba tuliokimbia nchi utukubalie kurejea bila masharti.Pia tulikuwa  na watu wengi waliokamatwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. 

“Tulikuomba waliokamatwa baada ya uchaguzi wote waachiwe na uliwaachia.Pia tulikuomba  mikutano ya hadhara ifunguliwe, uliruhusu kufunguliwa lakini kwa bahati mbaya tukaanza kukutukana."

Akieleza zaidi Wenje ambaye ana sıku ya tatu tangu kujiunga na CCM amefafanua katika kikosi kazi kilichoongozwa na Profesa Rwekaza Mukandala baada ya Rais Dk.Samia kukiunda kikosi kazi hicho kilichojumuisha wadau wa vyama vya siasa na watu mbalimbali mashuhuri.

“Dk.Samia alitoq mwito kwa wadau hao kukusanya maoni na kuwasilisha mapendekezo kuhusu hatua za kuchukua katika kuimarisha demokrasia nchini.CHADEMA hatukuja.

“Lakini tulileta mapendekezo kuomba marekebisho ya Ibara ya 7 katika Shetia ya Uchaguzi kuomba wakurugenzi wasiruhusiwe kusimamia uchaguzi. Mabadiljko hayo yakafanyika.

“Na leo nimezungumza na mwangalizi wa uchaguzi amesema amezunguka maeneo yote hakuna mahali kuna mkurugenzi hata mmoja wa halmashairi anasimamia uchaguzi.

“Pia tuliomba katika Uchaguzi Mkuu kusiwe na mgombea anayepitq bila kupingwa, sheria ikabadilishwa na leo hakuna mgombea atakayepita bila kupingwa. 

“Tuliomba namna viongozi wa tume ya uchaguzi wanavyochaguliwa, sheria ikaundwa ambapo sasa kuna kamati ya kumshauri Rais kuhusu uteuzi huo,”amesema Wenje na kuongeza “ Licha ya mabadiliko hayo CHADEMA ilikataa kushiriki uchaguzi kwa kwa uoga.”

Pamoja na hayo amesema ni hatari  sana kuongozwa na kiongozi anayesema yupo tayari kufa. Kama Musa angekufa katikati ya maji asingeweza kuwavusha wanaisrael. Hakuna matumaini katika kifo.

Hivyo amesema amejiunga na CCM baada ya kubaini kuwa katika maisha yake  yote kwenye siasa alikuwa akicheza Ndondo Cup, “Sasa nimekuja ligi kuu kucheza mpira mnene.”

Wenje ambaye moja ya sifa yake kubwa ni kujenga hoja amewaambia Watanzania katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kura zote ni kwa Dk.Samia Suluhu Hassan na kwamba kuanzia sasa mtu ukisalimiwa unajibu kwa kusema Oktoba 29 tuna tiki.

“Katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya uchaguzi mkuu mtu akikusalimia habari za leo wewe mujibu kwa kumwambia Oktoba 29 tunatiki.Hiyo ndio iwe salamu yetu.”




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad