HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 1, 2025

Dkt. Samia Azindua Kampeni za CCM Pwani, Agawa Ilani kwa Wagombea Ubunge

Na Mwandishi Wetu.

Pwani, Septemba 28, 2025: Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni zake kwa kukutana na wananchi wa Mkoa wa Pwani na kugawa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa wagombea ubunge wa mkoa huo.

Katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, Dkt. Samia aliwahimiza Watanzania kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa kuwa kimethibitisha uadilifu na ufanisi katika kuleta maendeleo ya Taifa.

"CCM imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kwa manufaa ya wananchi wote. Ilani tuliyoizindua ndiyo mkataba wetu wa kazi na Watanzania kwa miaka mitano ijayo," alisema Dkt. Samia.

Alisisitiza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka huu imejikita zaidi katika kuendeleza miradi ya miundombinu, huduma za kijamii, ajira kwa vijana, na kuimarisha uchumi shirikishi unaogusa maisha ya wananchi wa kawaida.

Wagombea ubunge wa CCM mkoani Pwani walipokea nakala za Ilani hiyo kwa ajili ya kuzitumia katika kampeni zao, wakiahidi kuisimamia ipasavyo endapo watapewa ridhaa na wananchi.

Kampeni za CCM zinaendelea mikoa mbalimbali nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku chama hicho kikiweka msisitizo kwenye mshikamano wa kitaifa, amani na maendeleo endelevu.
Sehemu ya wananchi wa Kibaha mkoani Pwani waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Septemba, 2025.
Shamra shamra za wananchi wa Kibaha mkoani Pwani katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Septemba, 2025.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad