HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 14, 2025

CHALINZE WAHAMASISHWA KUTUMIA VEMA TEHAMA


Na Khadija Kalili Michuzi TV
MKURUGENZI Msaidizi Sera Utafiti na Ubunifu TAMISEMI Lemmy Shumbusho ametoa wito kwa washiriki wa mafunzo ambao ni Viongozi Waandamizi na Wakuu wa Idara, Maafisa Waandamizi na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Chalinze kuwa wabunifu na kutumia teknolojia hasa katika kukusanya mapato kwa sababu inasema kweli na uwazi.

Shumbusho amesema hayo leo Oktoba 13, 2025 alipokuwa akifungua mafunzo hayo ya juma moja yanayofanyika kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Mkoani Pwani.

"Mafunzo haya ya Uongozi na Usimamizi ni sehemu ya jitihada endelevu za serikali katika kuboresha utendaji katika ngazi ya Halmashauri, uwekezaji katika ngazi ya uongozi ambayo ndiyo injini ya kuboresha utoaji wa huduma kuongeza uwajibikaji, kuimarisha nidhamu ya matumizi ya rasilimali na kusukuma mbele agenda ya maono kwa wananchi " amesema Shumbusho.

Aidha amewataka washiriki hao kuisoma na kuielewa vema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 nasisitiza ikawe ndiyo muongozo wenu wa kipa siku.

" Dira hii siyo nyaraka ya kukaa kabatini ni dira ya mabadiliko inayotaka tuweke matokeo ya wananchi mbele tuharakishe ubunifu , tuimarishe uwajibikaji na matumizi ya TEHAMA, na tuweke takwimu mbele ta kila maamuzi".

"Hivyo basi oanisheni mafunzo mnayopata hapa na Dira 2050 katika utekelezaji wa majukumu yenu kuanzia mipango Mikakati ya Idara , Mpango na bajeti wa mwaka , uchambuzi wa takwimu za NBS na Ofis ya Rais -TAMISEMI, hadi usimamizi wa miradi kipaumbele katika Halmashauri ya Chalinze.

Wakati huohuo amesema kuwa ni wajibu wa kila Idara kuwa na malengo yanayopimika na yanayoonekana kwa wananchi mfano barabara zinazopitika muda wote , huduma za maji zenye uwiano na mahitaji, ukusanyaji mapato wa kimfumo na usimamizi makini wa miradi ya afya , elimu na miradi mbalimbali ya kimkakati yenye lengo la kukuza uchumi wa Halmashauri ya Chalinze panga soma pima na chukua hatua za marekebisho mapema.

Wakati huohuo amewasisitiza kuwa na usimamizi shirikishi wa rasilimali za umma , utawala bora na uwajibikaji, kutumia takwimu katika maamuzi kwani kila Idara ina viashiria muhimu (KPIs), zitumiwe vizuri takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI na takwimu za ndani za Halmashauri bila takwimu tunategemea hisia kwa takwimu tunajenga maamuzi thabiti.

Pia amewataka kutumia vyema mifumo ya TEHAMA iliyopo nanitakayokuja katika ukusanyaji wa mapato, manunuzi, rasilimali watu na ufuatiliaji wa miradi.Dijitali si anasa ni njia ya kupunguza mianya ya upotevu , kuongeza uwazi na kuharakisha huduma pia viongozi na wataalamu mnapaswa kuhamasisha na kuendeleza ubunifu wa ndani ubunifu unaweza kujitokeza katika namna za kuboresha utaratibu wa utoaji huduma kutengeneza suluhisho za kiteknolojia rahisi kulingana na mazingira halisi ya Chalinze au kuanzisha mbinu za kiutendaji ambazo zinaboresha ushirikiano na wadau.

Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Shule ya Mwalimu Julius Nyerere Profesa Marcellina Mvula Chijoriga,John Baitani amesema kuwa mafunzo haya yatatolewa na Mkufunzi Balozi Mbobevu wa Diplomasia Omar Mjenga kwa kushirikiana na wakufunzi wengine.

"Mafunzi haya ni yatafanyika kati ya tarehe 13 hadi 18 Oktoba 2025" amesema Baitani.

Mbali ya masomo pia washiriki hupata muda wa kushiriki michezo mbalimbali katika viwanja vilivyopo pia kuna vyumba maalumu ambavyo hufanyika ibada kwa waumini wa dini zote pia kuna utulivu wa hali ya juu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad