MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Geita mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Chacha Wambura amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imemaliza kilio kilichodumu miaka 26 ya fidia kwa wananchi wa maeneo yanayozunguka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
Mhandisi Chacha ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM, Dk Samia Suluhu uliofanyika viwanja vya Dk Samia Bombambili mjini Geita.
"Amesema madai hayo ya fidia yalihusisha GGML na wananchi ambao walilalamikia maeneo yao kuwa ndani ya leseni ya kampuni hiyo ambapo hawakuwa na nafasi ya kuyaendeleza kwa kufanya shughuli za kiuchumi."
Amesema utatuzi wa kilio hicho umedhihirisha Dkt Samia anaongoza kwa kujali Utu wa watu na hiyo inaonyesha anastahili kupewa nafasi nyingine ya kuongoza taifa katika uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.
Kwa upande wake Waziri wa Madini na Mgombea ubunge wa jimbo la Mtumba mkoani Dodoma (CCM), Anthony Mavunde amesema mchakato wa tathimini ya fidia eneo hilo imefikia asilimia 92.
Mavunde amesema wanufaika wa fidia ni waathirika wote ambao ni wakazi wa Nyakabale, Nyamalembo, Ikumbayaga, Mizingamo pamoja na Magema Manispaa ya Geita mjini.
No comments:
Post a Comment