HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 22, 2025

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 527.751 kwa ajili ya kuhudumia jumla ya miradi 13 ya kitaifa kwa jumla ya kilomita 612.4, madaraja manne na mizani minne ya Kizengi miwili na Mizani ya Mkolye katika mkoa wa Tabora.

Mkoa wa Tabora una mtandao wa Barabara wa kilometa 2188.09, katika mtandao huo, Barabara kuu ni kilometa 1077.12 na Barabara za mkoa ni kilometa 1073.37 na kilomita 37.6 ni za Wilaya. Aidha jumla ya Kilomita 803.66 za Barabara kuu ni za kiwango cha lami na kilomita 273.46 ni za changarawe, kwa Barabara za mkoa kilomita 44.75 ni za lami na kilomita 1,028.62 ni za changarawe na kilomita 4 ni za kiwango cha lami na kilomita 33.6 ni za kiwango cha changarawe.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Octoba 2025 na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora Mhandisi Raphael Mlimaji ofisini kwake Mjini Tabora wakati akizungumzia miaka minne ya Rais Samia tangu aingie madarakani ambapo ameitaja miradi 7 iliyokamilika yenye thamani ya shilingi bilioni 488.152 pamoja na madaraja manne sawa na asilimia 92.5 huku miradi mingine 6 yenye thamani ya shilingi bilioni 39.598 sawa na asilimia 7.5 ikiwa inaendelea na hatua mbalimbali za ujenzi.

Ameitaja miradi ya Kitaifa iliyokamilika kuwa ni Pamoja na ujenzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Tabora ambao umefikia asilimia 97 unaotekelezwa na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group kwa shilingi bilioni 27.943 chini ya Mhandisi mshauri Khatibu&Alami Consulting Engineers Offshore S.A.L, ujenzi wa Barabara ya Nyahua – Chaya yenye urefu wa kilomita 85.4 na madaraja mawili (Nyahua na Kizengi) iliyojengwa na mkandarasi CHICO kwa gharama ya shilingi Bilioni 117.939 pamoja na ujenzi wa Barabara ya Usesula – Komanga yenye urefu wa kilomita 108 iliyojengwa na mkandarasi Jiangxi Geo Engineering Group chini ya Mhandisi mshauri Leah International Ltd iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 158.825

Mhandisi Mlimaji ameitaja miradi mingine iliyokamilika kuwa ni ujenzi wa Barabara ya Komanga – Kasinde yenye urefu wa kilomita 108 na daraja moja la Koga ul8ojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 140.025 na Ujenzi wa Barabara ya Kazilambwa – Chagu yenye urefu wa kilomita 36 kwa gharama ya shilingi Bilioni 48.652 zote zikiwa zimejengwa na mkandarasi CHINA WU YI Co Ltd chini ya Mhandisi Mshauri TECU.

Sambamba na hizo pia ujenzi wa mizani ya kizengi uliojengwa na mkandarasi China WuYi Co Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 15.058, ujenzi wa kilomita 1 katika Barabara ya Mambali – Bukene – Itobo yenye urefu wa kilomita 114 kwa gharama ya shilingi bilioni 1, ujenzi wa mita Daraja lenye mita 10 na Barabara za maingilio katika Barabara ya Ipole – Rungwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.650 ambapo miradi hii imeengwa na mkandarasi Salum Motor Transport Co. Ltd chini ya usimamizi wa mhandisi mshauri TECU.

Ameitaja miradi ambao imefanyiwa upembuzi na usanifu wa kina ni Barabara ya Puge – Ziba - Choma ambao umefikia asilimia 75 wenye urefu wa Kilomita kwa 109 kwa gharama ya shilingi milioni 494.350, mradi ujenzi wa Barabara ya Tabora – Ulyankulu ambayo imefikia asilimia 70 kwa gharama ya shilingi milioni 506.35 miradi hii inatekelezwa na mkandarasi NIB Plan Consult Ltd na msahauri elekezi akiwa ni TECU, Huku Barabara ya Tutuo – Usoke yenye urefu wa kilomita 69 ikiwa inatekelezwa na mhandisi Consultancy Limited umefikia asilimia 20.

Miradi mingine ni ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Inala – Ifucha yenye urefu wa kilomita 5.3 unaojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9,551.186 pamoja na ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami Tabora – Mambali – Bukene - Itobo kilimota 114 kipande cha mita 300 kwa gharama ya shilingi milioni 500 miradi yote hii inatekelezwa na mkandarasi Salum Motors Transport Limited na mhandisi mshauri akiwa ni TECU.

Sambamba na hayo Mhandisi Mlimaji amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 mpaka sasa 2025/2026 serikali imefanya na inaendelea kufanya matengenezo (Maintanance) kwenye madaraja 637 katika mtandao wa Barabara za mkoa wa Tabora unaohudumiwa ambapo jumla ya shilingi Bilioni 133.7 imepangwa kutumika.

Amesema kuwa kukamilika kwa maboresho ya uwanja wa ndege Tabora, Ujenzi wa Barabara na madaraja kutarahisisha huduma za biashara ndani na nje ya nchi, kupunguza muda wa usafiri na usafirishaji, Kukuza uchumi na kuongeza utalii, urahisi wa wananchi kufikia huduma za jamii Pamoja na kuipunguzia serikali gharama za mara kwa mara za matengezo ya Barabara.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad