RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Bill Gates usiku kuamkia leo Septemba 24, 2025 ambapo ameshiriki katika hafla ya “Goalkeepers” Jijini New York Marekani, iliyoandaliwa na Taasisi ya Bill Gates na kukutana na wadau mbalimbali.
Hafla hiyo ambayo ilihusu masuala ya afya ya watoto chini ya miaka mitano, ilikutanisha watu mashuhuri kutoka duniani kote.
Hafla hiyo ililenga kuendelea na uhamasishaji wa kuunga mkono uwekezaji katika afya kwa ujumla na maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment