Mheshimiwa Balozi Kombo ametoa mwaliko huo Agosti 21, 2025 nchini Japan alipokutana na kuzungumza na Shirikisho la kampuni za wawekezaji wa miundombinu la Japan (JAIDA) ambalo linajumuisha takriban kampuni 190 na Wenyeviti wenza wa Kamati ya Afrika ya Shirikisho la wawekezaji la KEINDAREN ambalo linajumuisha takriban kampuni 1,500.
Katika mazungumzo yake na wawekezaji hao, Mheshimiwa Waziri Kombo amesisitizia nia ya Tanzania ya kutumia ushirikiano wa Tanzania na Japan katika sekta za kimkakati kama alama kuu ya ushirikiano wa Japan na Afrika.
Vilevile, amesisitizia umuhimu wa kuongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan katika kuendeleza rasilimali watu ya Tanzania na kubadilishana ujuzi, uzoefu na teknolojia katika sekta mbalimbali za miundombinu, uzalishaji, viwanda na kilimo.
Kwa upande wa wawekezaji wa Japan wameahidi kutumia fursa hiyo na kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika uwekezaji na biashara kwa maslahi mapana ya pande zote mbili kupitia miradi ya PPP.


















No comments:
Post a Comment