Mheshimiwa Waziri Kombo amepongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia JICA katika ufadhili wa uendelezaji wa sekta za kilimo; nishati; usafirishaji; afya; maji na uendelezaji wa rasilimali watu.
Katika kikao hicho walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo hususan katika sekta za miundombinu bora, uendelezaji wa rasilimali watu; uchumi wa buluu na kilimo, hususan teknolojia ya kuongeza thamani malighafi za mazao.







No comments:
Post a Comment