HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 26, 2025

WAJA ACHUKUA FOMU YA UTEUZI JIMBO LA GEITA MJINI - "KAZI NA MATOKEO"

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini,CHACHA WAMBURA amechukua fomu ya uteuzi katika Ofisi za Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya GEITA eneo la Magogo.

Akizungumza baada ya kupokea fomu za uteuzi,mgombea huyo WAMBURA ameshukuru wagombea wenzake waliotia nia katika kugombea nafasi ya kuteuliwa kuweza kushirikiana nae katika hatua hii ya kuchaguliwa na Chama cha Mapinduzi kupeperusha bendera kugombea nafasi hiyo.

“Namshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Kamati Kuu kurudisha jina langu ambapo leo ndiyo maana nimekuja kuchukua fomu lakini jambo hili halikuwa na mchakato wa juu tu bali ilianzia chini kutokea kwenye kata ikaenda wilaya,mkoa na baadae katika halmashauri kuu ya taifa ambapo waliweza kurudisha jina langu”amesema Wambura

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa GEITA, NICHOLAUS KASENDAMILA amesema wanaoenda kugombea ni wanachama wote wa chama hicho ila mgombea yeye ndiye mshika bendera hivyo ameomba ushirikiano kwa wanachama wote kushirkiana na kuvunja makundi yote ambayo yalikuwa hapo awali na kuwa wamoja katika kipindi hiki.


Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita,NDARO SAMSONI amesema mwisho wa kurudisha fomu za uteuzi ni Tarehe 27 ya mwezi huu saa 10 jioni.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad