Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tume na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 01, 2025.

Na Avila Kakingo
VYOMBO vya habari nchini vimepewa jukumu la kipekee la kuwa kiungo kati ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na wananchi, ili kuhakikisha taarifa kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025 zinawafikia wananchi kwa usahihi, kwa wakati, na kwa lugha rahisi kueleweka.
Akizungumza leo Agosti 1, 2025 jijini Dar es Salaam katika kikao maalum cha Tume na wahariri wa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, amesema kuwa media ni mhimili usioepukika katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki, huru na wa amani.
"Vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kuwaelimisha wananchi kuhusu haki yao ya kupiga kura, na kuwaongoza kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia taarifa zilizohakikiwa," alisema Jaji Mwambegele.
Ameongeza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Tume na vyombo vya habari utasaidia kupambana na taarifa potofu, kuhimiza ushiriki mkubwa wa wapiga kura na kuimarisha uwajibikaji katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema kuwa bila mchango wa vyombo vya habari, jitihada za Tume kuwafikia wananchi zitakuwa na mapungufu makubwa.
"Media ndio sauti ya kwanza inayoweza kufichua upotoshaji au taarifa zisizo sahihi kuhusu uchaguzi. Ushirikiano nao ni lazima, si hiari," alisema Kailima.
Wahariri walioudhuria kikao hicho waliitaka Tume kuongeza fursa za mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari, si tu wakati wa uchaguzi, bali kama sehemu ya maandalizi endelevu. Pia walisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa vifaa vya kielimu kama sheria za uchaguzi, miongozo ya uandishi na nyenzo za uhamasishaji.
Joyce Shebe kutoka Clouds Media Group alisema, “Tunapewa elimu ili tuwaelimishe wananchi. Kila mwandishi ni daraja la maarifa kutoka Tume kwenda kwa mpiga kura.”
Kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu 2025, “Kura Yako, Haki Yako – Jitokeze Kupiga Kura”, imetajwa kuwa ni ujumbe muhimu wa kuendelezwa katika kila taarifa za habari kuelekea Oktoba 29, 2025.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg Kailima Ramadhani akitoa mada wakati wa Kikao cha Tume na wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agost 01, 2025.

Sehemu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakishiriki mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 01, 2025.

No comments:
Post a Comment