HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 1, 2025

Tume Yawahimiza Wahariri Kuvaa Koti la Uzalendo Katika Uchaguzi 2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tume na Wahariri wa Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 01, 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg Kailima Ramadhani akitoa mada wakati wa Kikao cha Tume na wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agost 01, 2025.


Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakishiriki mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 01, 2025.

Na Cathbert Kajuna - Dar es Salaam.

Wahariri wa vyombo vya habari nchini wameaswa kuhakikisha wanafuata kanuni na miongozo ya maadili ya uchaguzi bila kupendelea chama, mgombea au chombo chochote cha siasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mheshimiwa Jaji Jacobs Mwambegele, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wahariri na viongozi wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam.

“Vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kuleta uchaguzi wa amani, wa haki na wa huru. Tunawaomba wahariri kusimamia ukweli, uwajibikaji na kutotoa nafasi kwa habari zenye mwelekeo wa kichochezi au upendeleo,” alisema Jaji Mwambegele.

Mwenyekiti wa Tume amesisitiza kuwa, uchaguzi ni mchakato wa pamoja unaohitaji ushirikiano wa wadau wote: Serikali, vyombo vya habari, asasi za kiraia, na wananchi.

“Tukisimama pamoja, tukiheshimu sheria na maadili, tutashuhudia uchaguzi bora zaidi katika historia ya taifa letu,” alihitimisha Jaji Mwambegele.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad