HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 3, 2025

TAASISI YA UONGOZI YAPONGEZWA KWA KULETA MABADILIKO KATIKA UONGOZI KUPITIA PROGRAMU ZAKE MBALIMBALI

Na Said Mwishehe Michuzi TV

KATIBU Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said ameipongeza Taasisi ya Uongozi kwa kuwa na programu mbalimbali za kuwajengea uwezo viongozi wakiwemo Wanawake huku akisisitiza taasisi hiyo imelenga kuleta mabadiliko si tu ndani ya Tanzania bali ndani ya Afrika.

Aidha ametumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa viongozi wa taasisi mbalimbali nchini kuhakikisha inatumia taasisi hiyo kuwaandaa watu wake wakiwemo wale ambao wanatarajia kuwa viongozi ambapo pia amekumbusha viongozi kuchunga ndimi na matendo yao wawapo maeneo ya kazi au katika jamii zao.

Mhandisi Zena Said ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzinduliwa rasmi kwa Jukwaa la Wahitimu wa taasisi hiyo ambapo wahitimu 460 wamehudhuria kati ya wahitimu 860 ambao wamepita katika taasisi hiyo kupitia programu mbalimbali.

Mhandisi Zena Said amesema kwamba kwa muda mrefu sasa Taasisi ya Uongozi imefanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika uongozi kutokana na programu mbalimbali ambazo wamekuwa wakiziandaa kwa ajili ya viongozi sio tu Tanzania bali katika bara la Afrika .

"Taasisi ya Uongozi si tu inalenga kuleta mabadiliko ndani ya Tanzania lakini ndani ya Afrika.Tumeona programu mbalimbali zimekuwa zikitolewa na taasisi hiii ikiwemo programu ya kuwajengea uwezo viongozi wanawake ili waweze kujiamini na kusimama vema katika kutekeleza majukumu yao.

"Kuna ulazima wale ambao wanaandaliwa au wako katika orodha ya kusubiriq kuteuliwa kuwa viongozi kupita katikq taasisi hii wapikwe vizuri.Kati yenu wahitimu wengjne mmeshaingia katika kundi la uteuzi na ukweli hili ni jambo ambalo linatakiwa liwe lazima mamlaka iwe na sampuli ya watu ambao wako tayari wameshapikwa na wakipewa majukumu wanaweza kufanya vizuri

"Bila kuwa na watu walioandaliwa inakuwa ni kama ubahatisha,wakati mwingine anapatikana mtu mzuri wakati mwingine sio, hivyo ninyi ambao mmepita Taasisi ya Uongozi ni kama vile mmfeundwa yaani hapa naamini yeyote kati yenu akipewa fursa ya uongozi katika ngazi fulani hawezi kutuangusha."

Aidha amesisitiza kuna utofauti mkubwa kati ya waliopita Taasisi ya Uongozi na wale ambao hawajapita katika taasisi hiyo .Ni muhimu sana kupata mafunzo ya Taasisi ya Uongozi kwasababu tunaona viongozi mpaka unashangaa ,hivyo ambao wamepata mafunzo lazima wawe tofauti.”

Amesisitiza waliopita programu za uongozi lazima wawe tofauti na wakifanya hivyo itasaidia hata taasisi nyingine waone haja ya kupeleka watu wao Taasisi ya Uongozi kwasababu wanaona akitoka kwenye kozi yeyote ya uongozi amebadilika anakuwa tofauti.

Aidha Mhandisi Zena Said amewashauri viongozi na wale ambao wanasubiria nafasi za uongozi wachunge mdomo maana mdomo ni sumaku ya maneno unayosema ,unayojadili kwa yale unayotoka hata kama utani.

“Yaani ukikisema au umekitengaza kinaenda kule kwahiyo kama unajiona una majanga majanga yanajirudia hebu fikiria huwa unasema nini hata mwenyewe wakati mwingine wewe mwenyewe unadhani unafikiria unatani.”

Kuhusu programu za mafunzo kwa viongozi Wanawake,Mhandisi Zena Said amesema programu hizo angalau sasa zimefanya wanawake waonekane katika nafasi za maamuzi kwani huko nyuma kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakipuuzwa katika kuendelezwa kielimu na hata kwenye vyombo vya maamuzi.

“Tumeanza kuona wanawake wanaonekana kwahiyo kwa kiasi fulani mnaweza kuonekana na kwa namna fulani wanawake wanaweza kuonekana tishio kwa wanaume lakini nawaomba niwape neno lengo kubwa ni kuwajengea uwezo Wanawake wa kujiamini katika nafasi za uongozi na kujengewa uwezo huu haina maana wanataka kulipa kisasi kutokana na uwepo wa mfumo dume.

“Mwanamke anapopewa nafasi ya kujiendeleza kielimu lakini pia na kupata mafunzo ya uongozi maana yake kubwa ni kumfanya awe anajitambua na kujiamini na kubwa zaidi wawe na fursa ya kushiriki katika maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.”

Kuhusu Dira ya 2050,Mhandisi Zena Said ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa kuna kila sababu ya wananchi wote kushiriki kikamilifu katika kuifanikisha dira hiyo kwani kwa walioko Serikalini wanafahamu kila mmoja katika sekta yake anatakiwa kufanya nini.

“ Nimekuwa najiuliza swali moja hivi wananchi wanajua wanatekelezaje dira au wanafikiri inatekelezwa tu na serikali? Nafikiri tujiulize hilo, kwani viongozi serikali sio wengi lakini wananchi ndio wengi.Kwahiyo Dira 2050 ni vema mwananchi mmoja mmoja ajue wajibu wake ni upi katika kuhakikisha tunafikia.”

Amesisitiza kwamba dira hiyo imezingatia maoni ya wananchi kupitia makundi mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa mchakato wake hivyo katika kuifanikisha lazıma nchi itembee kwa pamoja na kusisitiza lengo la Serikali ni kuona utekelezaji wake unakwenda mpaka ngazi ya chini kabisa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Kadari Singo ameeleza kwa kina sababu za kuanzishwa kwa Jukwaa la Wahitimu wa taasisi hiyo ambapo amesema kubwa ni kutumia jukwaa hilo kubadilishana uzoefu na kurudisha fadhila kwa kile walichokipata katika mafunzo ya uongozi.

“Tumeanzisha jukwaa hili kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali kwani tunatambua wako wengi ambao wamepata mafunzo ya uongozi katika taasisi hii.Lakini tutawatumia wahitimu hawa kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wengine ambao watakuwa wanakuja katika programu zetu.”

Pia amesema wako katika mchakato wa kuanzisha programu mpya ya viongozi chipukizi ajili ya kuwaanda mapema wakiwa wachanga ili wanapokuja kushika nafasi mbalimbali za uongozi wazitumikie vema.

Kuhusu jukwaa la Wahitimu amesema sio la taasisi ni la Wahitimu wenyewe ambao wameamua kuwa na jukwaa lao lakini wao kama Taasisi wameona haja ya kuwa nao katika kuhakikisha linafanikiwa na watakuwa wanakutana mara moja kwa mwaka huku akifafanua wahitimu waliopita katika taasisi ni 860 na waliohudhuria ni 460.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad