HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 14, 2025

Prof. Kahyarara: Tumejipanga Kutekeleza Maagizo ya Rais Kuhusu Bandari Kavu

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara akizungumza wakati akifungua  kikao cha watalaam kujadili mikakati ya utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya Bandari Kavu ya Kwala katika kuhudumia shehena ya Bandari ya Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa agizo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuhamishia shughuli za shehena katika Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani.
Rais wa Mawaka wa Forodha Tanzania Edwad Urio akizungumza kuhusiana wadau wa forodha walivyojipanga katika uondoshaji wa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani.

Baadhi ya Matukio katika picha katika kikao

*Ni katika kuhudumia Shehena ya Bandari ya Dar es Salaam kupunguza msongamano.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, leo tarehe 14 Agosti, 2025 amefungua kikao cha watalaam kujadili mikakati ya utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya Bandari Kavu ya Kwala katika kuhudumia shehena ya Bandari ya Dar es Salaam, ambayo aliyatoa wakati wa ufunguzi wa Bandari Kavu ya Kwala uliofanyika tarehe 31 Julai, 2025.

Akizungumza katika kikao hicho kilichoitishwa na TASAC (mdhibiti wa usafiri majini) Prof. Kahyarara amesema kuwa Wizara inahakikisha utekelezaji wa maagizo hayo yanafanyiwa kazi kikamilifu kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo suala la foleni.

Prof. Kahyarara alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau hao na kuongeza kuwa uwekezaji katika Bandari Kavu ya Kwala iliyoko Kibaha Mkoa wa Pwani, utachangia si tu kuboresha usafirishaji, bali pia kufungua fursa nyingi za kiuchumi kwa sekta binafsi hapa nchini.

"Nyie kama wataalam, maoni yenu ni muhimu, hivyo, naomba tumieni fursa hii kujadili na kutoa mikakati ya utekelezaji wa maelekezo haya ili tuondoe suala la foleni katika jiji la Dar es Salaam ambazo zinasababishwa na malori yanayoingia na kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam,” ameongeza Prof. Kahyarara.

Kwa upande wa TASAC, Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mohamed Salum amesema kuwa dhima ya kikao hicho ni kuwakutanisha wadau ili kupata maoni yao kwa lengo la kujadili namna bora ya kuchangia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Rais kuhusu matumizi ya Bandari Kavu ya Kwala katika kuhudumia shehena ya Bandari ya Dar es Salaam.

Nae, Rais wa Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Bw. Edward Urio amesema kuwa wameshajiandaa na wanaendelea kufanya kazi katika Bandari Kavu ya Kwala na kushauri nguvu zaidi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutumia Bandari ya Kavu ya Kwala.

Bw. Urio ameshauri TRC kutumia fursa ya kubeba mzigo wa shaba kutoka nchi jirani ili kupunguza malori kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad