HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 1, 2025

NDANI YA MUDA MFUPI HATUTAAGIZA BIDHAA KUTOKA NJE :DKT JAFO

 



WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selamani Jafo ameeleza kuwa, ndani ya muda mfupi hakutakuwa na haja ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kama vile bidhaa za mabati, vioo, nondo na saruji

Waziri Jafo ‎amebainisha hayo wakati wa ziara ya Rais Samia Julai 31,2025 mkoani Pwani ambapo alikuwa anafanya uzinduzi wa kongani ya Viwanda Kwala, sambamba na uzinduzi wa bandari kavu ya kwala.

‎"Ndani ya muda mfupi kuanzia sasa hakutakuwa na haja ya kuagiza bidhaa tena kutoka nje kwa mfano, mahitaji ya mabati kwa mwaka ni tani laki moja na elfu thelathini, leo hii makampuni yote yanayozalisha bidhaa hiyo ikiwamo ya Lodhia, king Lion,Alaf n.k imeweza kufikia tani laki 2 na elfu 60 inamaana tunaakiba ya tani laki moja na elfu thelathini."

‎Aidha, ameeleza kwa lengo la kutaka kupunguza uingizaji wa bidhaa na kuongeza usafirishaji kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara, itasimamia maono ya. Rais Samia kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi kinara kwa uzalishaji wa bidhaa, kusafirisha nje ya nchi na kuingiza fedha za kigeni.

‎"Eneo la viwanda kwala lenye zaidi ya hekta 1000 zaidi ya viwanda 200 vitajengwa ambavyo uwekezaji wake ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni tatu ambayo kwa mwaka mauzo yatakayopatikana kwa bidhaa zitakazozalishwa ni takribani bilioni sita ambazo kati ya hizo bilioni mbili kwa usambazaji na bilioni nne kwajili ya matumizi ya ndani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad