Hayo yamebainishwa wakati wa kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa Takeshi Iwaya kilichofanyika pembezoni mwa Mkutano wa TICAD 9 jijini Yokohama Agosti 21, 2025.
Viongozi hao pia wameahidi kuendelea kushirikiana katika masuala ya kimataifa, hususan kwenye agenda zenye manufaa kwa pande zote na utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa njia ya ubia wa sekta ya umma na binafsi.




No comments:
Post a Comment