Wazee wa Roto, Mabasi FC kutoka mjini Kahama, wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Mapung’o Cup 2025 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Casablanca FC ya Bukoli.
Matokeo hayo yamewapa Mabasi FC nafasi ya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2, wakitumia faida ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza.
Kocha wa Mabasi FC, Hussein Eliasi, amesema timu yake imejipanga kuhakikisha inafika fainali na kuchukua kombe, akisisitiza kuwa desturi yao siyo kuishia njiani kwenye mashindano, bali kufika mwisho kwa ushindi.
Viongozi wa Casablanca FC ya BUKOLI walitokomea baada ya MCHEZO kuisha hawakuwa tayari kuongea na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment