KAMPUNI
ya LUNA Trading and Logistics Ltd imeendelea kupeperusha vyema bendera
ya Tanzania baada ya kutunukiwa tuzo ya kuwa kampuni ya kwanza ya
kizalendo nchini kwa mchango wake mkubwa katika kuunga mkono biashara ya
bidhaa za kilimo duniani.
Tuzo hiyo imetolewa hivi karibuni na
Afro World Agri-food International, taasisi inayotambua juhudi za
taasisi na mashirika yanayochochea ustawi wa kilimo na biashara ya mazao
ya kilimo katika bara la Afrika na kwingineko.
Akizungumza baada
ya kupokea tuzo hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa
LUNA Trading and Logistics Ltd, Nuru Mmanyi, alisema tuzo hiyo ni
uthibitisho wa dhamira ya kampuni hiyo katika kukuza uchumi wa kilimo
kwa kusaidia wakulima kupata masoko ya uhakika kimataifa.
“Tumejikita
kuhakikisha mazao ya kilimo kutoka Tanzania yanapata masoko ya nje ya
nchi kwa bei shindani. Hili sio tu linawanufaisha wakulima bali pia
linainua thamani ya mazao yetu katika soko la dunia,” alisema.
Aidha
Mkurugenzi wa kampuni hiyo ameipongeza serikali kwa kuweka mazingira
rafiki ya biashara hali inayopelekea kampuni za usafirisha nchini
kustawi.
LUNA imekuwa ikisafirisha kwa mafanikio mazao
mbalimbali ya kilimo kutoka Tanzania kwenda masoko ya nje, hasa katika
nchi za Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia na Amerika.
Bwana Mmanyi
amsema ampuni hiyo inashirikiana kwa ukaribu na wakulima kupitia vikundi
na vyama vya ushirika ili kuhakikisha mazao yanavunwa, kuchakatwa na
kusafirishwa kwa viwango vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment