Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI Dkt. Marina Njelekela ameipongeza menejimenti ya MOI kwa uamuzi wake wa kushiriki na kutoa huduma kwa washiriki wa mkutano wa wenyeviti wa bodi na wakuu wa Taasisi unaofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha.
Dkt. Njelekela ametoa pongezi hizo Leo 25/08/2025 alipotembelea eneo la kutolea huduma la MOI katika ukumbi wa AICC
“Nawapongeza menejimenti nzima ya MOI ikiongozwa na Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ukisubisya kwa uamuzi huu mzuri wenye tija wa kuja kutoa huduma kwa ashiriki wa mkutano huu mkubwa na muhimu, hongereni sana “ Alisema Dkt. Njelekela
Pia , Dkt Njelekela amepongeza ushirikiano kati ya Taasisi ya MOI, Taasisi ya Moyo JKCI na Hospitali ya AICC katika kuwahudumia washiriki wa mkutano huo.
Awali, Mkurugenzi mtendaji wa MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya alimuarifu Dkt. Njelekela kwamba MOI imeleta madaktari bingwa wa mifupa, Ubongo, Mgongo, viungo na mishipa ya fahamu ili watoe huduma za ushauri (Consultation) kwa washiriki wa mkutano huo ambapo wale watakaohitaji uchunguzi zaidi watapewa rufaa kwenda MOI
Taasisi ya MOI imeanza kutoa huduma kwenye kikao kazi cha Wenyeviti wa bodi na wakuu wa Taasisi za umma 2025 jijini Arusha kuanzia Agosti 23, 2025 na kutamati Agosti 26, 2025.







No comments:
Post a Comment