HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 4, 2025

WAZIRI KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI-HABARI-JAB

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana naWenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) alipotembelea Banda la Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB lililopo katika Kijiji cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Julai 04, 2025 jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika Banda hilo Mhe. Kikwete amekutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Wakili Patrick Kipangula (wa pili kutoka kushoto) aliyemuelezea historia fupi ya kuanzishwa Bodi hiyo, majukumu yake na maendeleo ya zoezi la usajili wa Waandishi wa Habari na ugawaji wa vitambulisho vya uandishi wa habari kwa waliokidhi vigezo vya kisheria.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mara baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB lililopo katika Wizara hiyo Julai 04, 2025 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana naWenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na viongozi mara baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB lililopo katika Kijiji cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Julai 04, 2025 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad