HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 1, 2025

KADA WA CCM, NDUGU MAGEMBE NONI, ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE WA JIMBO LA GEITA MJINI

Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Magembe Noni, ambaye ni mzaliwa wa Geita, amechukua rasmi fomu ya kuwania uteuzi wa chama chake kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini katika uchaguzi ujao.
Ndugu Magembe Noni ni mtaalamu wa jiolojia mwenye uzoefu mpana katika masuala ya uongozi, usimamizi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Ni mzalendo ambaye ameamua kutumia maarifa na muda wake kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa, ikiwa ni pamoja na kushiriki utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya serikali.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) uliokamilika kwa mafanikio makubwa, pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo Mkubwa wa Kilovoti 400 (400kV) unaounganisha Gridi ya Taifa ya Tanzania na ile ya Zambia kupitia Mradi wa TAZA.
Baada ya mchango wake mkubwa kwa taifa, Ndugu Magembe sasa amerudi nyumbani Geita, akiwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kama mbunge, ikiwa atapewa ridhaa na chama chake na baadaye kuungwa mkono na wananchi.
Katika maelezo yake, amesema lengo lake ni kushirikiana na wananchi kuharakisha maendeleo, kuimarisha uwakilishi wa kweli, na kutumia ujuzi alionao kushirikiana na serikali katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Geita Mjini.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad