HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 4, 2025

FCC Yawakaribisha Wananchi Kujifunza Kutambua Bidhaa Bandia Kwenye banda lao Sabasaba

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija Juma Ngasongwa amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji nchini, kusaidia kuimarisha biashara nchini, kulinda

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 4 julai 2025 alipofanya ziara kwenye banda la viwanda na biashara katika maonyesho ya 49 ya biashara sabasaba

" Sisi tupo hapa kutekeleza kuendeleza na kutimizaya Rais wa jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hali ya biashara nchini Tanzania " alisema bi. Hadija

Aidha alisistiza lengo la kuanzishwa tume ya ushindani ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda na kuhimarisha walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara nchini kati ya kampuni na kampuni, pamoja na kudhibiti bidhaa bandia.

Awali bi. Hadija Juma alisema lengo kubwa ni kuhakikisha uwekezaji ndani ya nchi waone kwamba kunasheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanaofanya.

" Tunajivunia na tunashukuru sana serikali kuweza kutengeneza mazingira sahihi ya wawekezaji kuhakikisha kwamba mwekezaji wa ndani kuweza kupata fursa zinazopatikana na ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri yaliyowekwa katika serikali yetu" alisema Hadija

Pia aliongezea wameweza kushiriki katika maonyesho ya sabasaba ni fahari kwao na kuwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho kuchukua fursa zaidi ya makampuni 3000 yanayopatikana kwenye banda la viwanda na biashara.

Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara

Aidha alisistiza kuna sheria ambayo ya kudhibiti bidhaa bandia, ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la viwanda na biashara kufika ili waweze kutofautisha bidhaa bandia na halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad