HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 4, 2025

Bodi ya TASAC Yatoa Suluhisho ya Kupunguza Mlundikano wa Makasha Bandari ya Dar es Salaam

 

Bodi ya TASAC ikipata maelezo katika bandari Kavu ya Kwala wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara katika Bandari hiyo.
Bodi ya TASAC ikipata maelezo katika bandari ya Dar es Salaam upande wa DP World wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara katika Bandari hiyo.
Bodi ya TASAC ikipata maelezo katika bandari ya Dar es Salaam upande wa DP World wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara katika Bandari hiyo.
Bodi ya TASAC katika Kikao na DP World
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC  Nahodha Mussa Mandia akizungumza katika kikao cha kupunguza mlundikano makasha katika Bandari ya Dar es Salaam upande wa DP World.


Matukio  katika picha wakati ziara ya Bodi ya TASAC katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu ya Kwala.

*Yakutanisha TPA na TRC katika uondoshaji wa makasha kwenda Bandari Kavu ya Kwala.


Na Mwandishi Wetu
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekutanisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) katika kutoa suluhisho ya uondoaji wa shenena za makasha katika Banadari ya Dar es Salaam kwenda katika Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani.

Hatua hiyo imetokana Bandari ya Dar es Salaam kuzidiwa na makasha ambapo makasha hayo husafirishwa kwa njia ya reli kutoka Dar es Salaam kwenda Bandari Kavu ya Kwala.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya ziara ya Bodi hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia amesema kuwa changamoto zilizokuwa zinasababisha ucheleweshaji wa makasha katika Bandari ya Dar es Salaam ni mawasiliano kati ya Bandari na TRC.

Amesema kuwa katika ziara hiyo wamekubaliana katika ushirikiano wa pamoja katika ya TPA na TRC katika kuondoa makasha hayo kuanzia sasa kwa kuanza kuondoa makasha 20 na baadae kufika 40 hali itayopunguza mlundikano wa makasha katika bandari ya Dar es Salaam.

Nahodha Mandia amesema kuwa Bodi baada ya kufanya ziara na kuona changamoto hizo watajielekeza kufatilia hatua kwa hatua kwa kile walichokiona.

Hata hivyo amesema kuwa kazi ya TRC ni kusafirisha makasha hayo kutokana na kuwa na vipaumbele vya kutoa huduma za usafirishaji ambapo makasha hayo pia ni sehemu ya kuongeza mapato ya Shirika.

Mwenyekiti wa Bodi wa TRC Ally Karavina amesema kuwa TRC wako tayari katika kwenda na kasi ya uondishaji wa makasha kutoka Dar es Salaam kwenda kwenda Bandari Kavu ya Kwala.

Karavina amesema kuwa TRC kutokana na uhitaji wa uondoshaji wa makasha katika bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari Kavu wataongeza nguvu zaidi ya kuongeza mabehewa kutoka 20 hadi 40.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Abeid Gallus amesema kuwa watashughulika zaidi na mawasiliano katika kuondoa makasha hayo kwa wadau wanaohusika.

Amesema bandari sio sehemu ya kuhifadhi makasha bali ni sehemu kupokea na kuondosha makasha hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad