Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule 1 ya Bweni ya Wasichana ya Mkoa, ujenzi wa shule ya 1 ya bweni ya Wavulana ya kanda, ujenzi wa shule 1 ya Amali ya Mkoa, ujenzi wa Shule 3 za Amali za Wilaya, ujenzi wa nyumba 18 za walimu, ujenzi wa mabweni 11, madarasa 18 na matundu ya vyoo 52 katika shule za Sekondari.
Pia kupitia programu hiyo ya SEQUIP serikali imetoa Shilingi Bilioni 35.791 katika mkoa wa Pwani ambazo zimetumika kukarabati shule kongwe, kujenga shule mpya za kata, shule ya Wasichana, shule ya kanda ya wavulana, mabweni, madarasa na matundu ya vyoo katika shule za Sekondari.
Vilevile Katika utekelezaji wa mradi huo serikali imejenga nyumba za walimu katika shule 12 za kata za awamu ya kwanza (2 in1), ujenzi wa bweni, ukarabati wa maboma ya madarasa, ukarabati wa maboma ya maabara na ukarabati wa maboma ya matundu ya vyoo.
Pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa shule 11 za sekondari za kata, shule 2 za Amali za kitaifa zilizopo Rufiji na Chalinze, na ujenzi wa shule 4 za amali za kawaida awamu ya kwanza. Vilevile upanuzi wa shule za sekondari ziwe za kidato cha tano, na kuongeza mabweni, Ujenzi wa madarasa 30, mabweni 25 na matundu ya vyoo 116 kwenye shule 12 za sekondari.










No comments:
Post a Comment