MAGEMBE NONI kipenzi cha wana Geita, Mzalendo aliyebeba maono ya jimbo la Geita mjini leo amekamilisha rasmi zoezi la urejeshaji wa fomu ya kuwania uteuzi wa kugombea ubunge kupitia CCM.
Hatua yake ya kutia nia imeibuwa matumaini mapya kwa wananchi wa jimbo la Geita mjini ambalo lina mvutano mkubwa wa watia nia vigogo.
Wakati NONI akirejesha fomu yake imepokelewa na Katibu wa CCM wilaya ya GEITA,MICHAEL MSUYA. Zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzli ilianza Mwezi Juni 28,2025 na kuhitimishwa leo Julai 2,2025 majira ya saa 10 jioni.
No comments:
Post a Comment