HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 6, 2025

WANAFUNZI KISIWANI WAELIMISHWA KUHUSU MATUMIZI SALAMA YA GESI

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas imeadhimisha Siku ya Mazingira duniani kwa kufanya usafi, kupanda miti, kukabidhi vifaa vya kuhifadhi taka na kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia katika shule ya msingi Kisiwani iliyopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam

Akizungumza katika Juni 5, 2025 katika zoezi hilo, Meneja Miradi Nishati Safi ya Kupikia wa kampuni hiyo Peter Ndomba amesema kuna kila sababu ya kuendelea kutunza mazingira kwa kutokata miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

“Leo(jana) dunia nzima inaadhimisha siku ya utunzaji mazingira wa bora,hivyo Oryx Gas tunachukulia mazingira kwenye upande wa misitu na miti,kwa kupitia hii bidhaa yetu ya gesi tunawashauri Watanzania wote wasiendelee kukata miti.

“Sasa hivi kuna juhudi kubwa za Serikali kwenye kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na moja ya lengo ni kuhakikisha mazingira yetu yako salama.Tanzania tunabahati kidogo tumebakiwa na misitu lakini wenzetu hawana.

“Lakini kwa nini tumekuja hapa Shule ya Msingi Kisiwani ,hawa ni watoto wadogo wanajifunza kila siku tumefanya nao usafi,tumewafundisha matumizi ya nishati safi maana wao hawana uwezo wa kununua gesi lakini wanakaa na wazazi wanapokuwa nyumbani.”

Amesema hivyo kampuni hiyo inaamini elimu ambayo wameitoa kwa wanafunzi hao ya kutumia gesi kwa usalama wataipeleka kwa wazazi wao na kusisitiza wamewaeleza kwanini kuna umuhimu wa kutunza miti.

“Sasa hivi hali ya hewa imebadilika mvua inanyesha tu, huu ni mwezi wa sita lakini mvua bado zinanyesha na sababu  hali ya hewa imebadilika kwa nchi nyingi duniani.Hivyo Watanzania tunawajibu kuendelea kutunza mazingira na tunarithisha kwa kizazi hiki cha watoto hawa. 

“Lakini tumewapa elimu hii kwa kutambua wakiipata mapema itasaidia kuwa na jamii inayotambua umuhimu wa kutunza mazingira badala ya kuipata elimu hii wakiwa wakubwa.Katika hii siku ya mazingira duniani sisi Oryx kwa kushirikiana na wadau wengine tunawahamsisha wananchi wasiharibu mazingira na kutoharibu mazingira.”

Amefafanua na kutoharibu mazingira ni kuwa na njia mbadala ya kutunza mazingira kama kuwa na nishati safi ya kupikia.Hivyo wanapotoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia wanalenga kuondoa uharibifu wa mazingira“Kwahiyo tunatumia siku ya leo kuwakumbusha watu mazingira ndio maisha bila mazingira bora hatuna maisha.”

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisiwani Abbas Degelo ameishukuru kampuni hiyo kwa kuungana na shule hiyo kufanya usafi wa mazingira ya shule hiyo sambamba na kukabidhi vifaa vya kuhifadhia taka.

“Nitoe shukrani nyingi kwa Oryx Gas kwa kutushirikisha  katika usafi wa mazingira hivyo kusaidia kutengeneza mazingira ya shule kuwa masafi.Naomba jamii pia itumie nishati safi ya kupikia ambayo ni marafiki wa mazingira lakini gharama ya gesi iko chini ukilinganisha kuni na mkaa.

Wakati huo huo wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwani wakiongozwa na Dada Mkuu Abigael Baraka na Mwakilishi wa Kaka Mkuu wa shule hiyo Gerevas Yusufu wamesema wanashukuru kwa kupata elimu ya matumizi salama ya nishati safi pamoja na kufanya usafi wa mazingira ambapo wameahidi watakuwa mabalozi wa kufikisha elimu hiyo kwa wengine ili kuwa na jamii yenye mtazamo mmoja katika kutunza mazingira.






















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad