Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia Makubaliano na Tume ya TEHAMA kwa ajili ya kuendeleza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika vyuo saba vya VETA vya wilaya kwa kipindi cha miaka mitano.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hay oleo, tarehe 20 Juni 2025, Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore amesema kuwa Tume ya TEHAMA itasaidi katika kuongeza ujuzi katika masuala ya Teknolojia kwenye vyuo vya VETA.
Amesema kuwa suala la Teknolojia linakuwa kila siku hivyo ni fursa ya vijana kupata ujuzi wa teknolojia ya TEHAMA kabla ya kuingia katika soko la ajira.
Amevitaja vyuo saba vitavyonufaika na makubaliano ya mafunzo ya TEHAMA ni katika Wilaya za Mpanda, Singida, Njombe, Morogoro, Songea, Mpanda pamoja na Singida.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema kazi ya tume yake itakuwa ni kuweka vifaa vya TEHAMA katika karakana za vyuo hivyo.
Dkt. Masaga amesema kuwa moja ya majukumu ya Tume ya hiyo ni kuendeleza TEHAMA nchini ambapo vijana ndio fursa yao kuingia na kuonyesha ubunifu.
No comments:
Post a Comment